Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apps 5 Kama FaceApp za Kutengeneza Sura ya Kizee (Android & iOS)

App hizi zina uwezo wa kubadilisha Picha za sura yako kuwa ya kizee
Apps 5 Kama FaceApp za Kutengeneza Sura ya Kizee (Android & iOS) Apps 5 Kama FaceApp za Kutengeneza Sura ya Kizee (Android & iOS)
<a href="https://www.themoscowtimes.com/2019/07/18/us-senator-asks-fbi-to-investigate-russias-faceapp-over-security-concerns-a66460" rel="nofollow noopener noreferrer" target="_blank"><span style="font-size: x-small">Photo via The Moscow Times</span></a>

Kama wewe ni mfuatiliaji wa mitandao mbalimbali ya kijamii, siku za karibuni lazima utakuwa umeona picha mbalimbali za sura za kizee za watu mbalimbali unao wafahamu. Kama ulikuwa unajiuliza kulikoni basi picha hizo nyingi zime tengenezwa kwa kutumia mfumo wa AI kupitia app inayoitwa FaceApp.

Sasa kuna baadhi ya watu ambao kutumia app ya FaceApp imekuwa ni mtihani kwa namna moja ama nyingine au inawezekana app hiyo haikufanya kazi vizuri kwenye simu yako. Kupitia makala hii nitakuonyesha apps nyingine 5 ambazo zinafanya kazi kama FaceApp na zinaweza kubadilisha picha ya sura yako kuwa ya kizee, Apps hizi ni rahisi kutumia na zinafanya kazi kwa asilimia 100. Bila kupoteza muda zaidi twende tukangalie apps hizi.

Advertisement

AgingBooth

AgingBooth
Price: Free
‎AgingBooth
Price: Free

AgingBooth ni app nzuri sana inapokuja kwenye swala la kubadilisha sura kuwa ya kizee, app hii ni nzuri na ukweli inaweza kukaribiana kabisa na app ya FaceApp. Uzuri wa app hii ni kuwa unaweza kubadilisha sura yako kupita mifumo yote ya Android na iOS.

Oldify

‎Oldify - Old Face App
Price: $0.99+

Oldify ni app nyingine nzuri sana ya kubadilisha sura kwenye picha zako kuwa ya kizee, app hii inafanana sana na FaceApp hivyo unaweza kutumia app hii kirahisi sana kama ushawahi kutumia app ya faceApp. App hii pia inakuja na effect nyingi sana hivyo jaribu kwenye simu yako kisha tupe maoni yako unaonaje app hii.

Face Changer Photo Gender Editor

Face Changer Photo Gender Editor ni app nyingine nzuri sana ya kubadilisha sura kuwa ya kizee, app hii inakuja na sehemu nyingine ya kubadilisha sura kuwa ya mwanamke kuwa mwanaume au mwanaume kuwa mwanamke, mbali na hayo kuna sehemu nyingine nyingi sana za kufanya ufurahie picha zako kwa namna tofauti.

Make Me Old

Make Me Old
Price: Free

App nyingine nzuri kwa ajili ya kubadilisha sura kuwa kama ya kizee ni app hii ya Make Me Old, app hii ni bora na haina tofauti na app nyingine kwenye list hii. App hii pia ni rahisi kutumia na inakuja na effect nyingi za kufanya ushangae sura yako.

Old Face

Old Face
Price: Free

App ya mwisho kwenye list hii inaitwa Old Face, App hii ni bora na inafanya kazi kama app nyingine kwenye list hii. Uzuri wa app hii ni kuwa inakuja na mfumo ambao unafanya ngozi ya uso wako kwenye picha kuonekana kama ya kwako kabisa tofauti na app nyingine kwenye list hii.

Na hizo ndio app nzuri ambazo zinafanana kwa namna moja ama nyingine na app ya FaceApp, kama kwa namna moja ama nyingine unataka kujaribu app ya FaceApp yenyewe basi unaweza kupakua app hiyo Hapa. Kama unataka kujua app nyingine nzuri unaweza kuendelea kusoma hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use