Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apps Nzuri za Kuedit Video Kwa ajili ya YouTube (Android)

Tumia app hizi kutengeneza video bora kwaajili ya YouTube
Apps Nzuri za Kuedit Video Kwa ajili ya YouTube (Android) Apps Nzuri za Kuedit Video Kwa ajili ya YouTube (Android)

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatumia mtandao wa YouTube basi ni vyema kufahamu kuhusu mabadiliko mapya kwenye mtandao wa YouTube. Lakini baada ya kusoma kuhusu vigezo hivyo na masharti, basi ni wakati wa kurudi kwenye “Game” na kuendelea kutengeneza video zaidi.

Kupitia makala hii nitaenda kushare na wewe app nzuri ambazo zinaweza kukusaidia kuedit video zako kwenye simu yako ya Android kwa urahisi na kuweza kukupa video zenye ubora sana kiasi kwamba watu wasiamini kama zimetengenezwa kwa kutumia simu.

Advertisement

Baada ya kujifunza kuhusu mambo ya muhimu ya kuzingatia wakati wa kurekodi video kwa simu, hebu sasa tungalie app zitakazo kusaidia ku-edit video zako vizuri baada ya kurekodi.

FilmoraGo ni app nzuri sana kama unataka kuedt video yako kwa urahisi kupitia simu yako ya Android. App hii inakuja na vitu mbalimbali kama vile uwezo wa kuweka slow motion kwenye video, uwezo wa kuweka filter mbalimbali ikiwa pamoja na uwezo wa kutengeneza video zenye format ya 16:9 video (YouTube).

Adobe Premiere Rush ni app nyingine nzuri sana ya ku-edit video kwenye simu yako, app hii kama lilivyo jina lake inatoka kwa Adobe hivyo lazima unajua itakuwa na uwezo mkubwa wa kuedit video kwenye simu, uzuri wa app hii ni kuwa inauwezo wa kutengeneza video yenyewe kwa kutumia picha na video zako utazo chagua. Mbali na hayo app hii inakuja na sehemu nyingi nzuri kwaajili ya mtu yoyote anayetaka kutengeneza video bora.

Kama ulikuwa umezoea ku-edit video kwenye kompyuta na ungependa kupata muonekano kama wa programu za kuedit za kompyuta kwenye simu yako ya Android basi app hii ya  PowerDirector  ni app nzuri sana kwako. App hii pia inakuja na sehemu nyingine nyingi ambazo unaweza kuzifurahia.

Sidhani kama kuna haja ya kuongelea sana kuhusu Kine Master, programu hii inatumiwa na watu wengi sana hapa Tanzania lakini kama bado hujawahi kutumia programu hii basi ni wakati wako wa kujaribu sasa. App hii inakupa sehemu nyingi sana za kuedit video zako ikiwa pamoja na kuweka transitions, na special effects.

Magisto ni app nyingine nzuri ya kusaidia kutengeneza video bora za YouTube, pia kupitia app hii unaweza kupata muziki wa bure kwaajili ya kuweka kwenye video zako ikiwa pamoja na effect mbalimbali za kuweka kwenye video zako. Kama unataka app rahisi kutumia ya kutengeneza video za YouTube basi jaribu app hii.

Video Show ni app nyingine nzuri sana ya kuedit video, app hii ni nzuri sana kwa sababu inakupa uwezo wa kutengeneza video zaidi ya video za YouTube. Kupitia app hii utaweza kutengeneza video kwaajili ya Instagram pamoja na mitandao mingine, pia unaweza kuweka effect mbalimbali kwa urahisi kupitia app hiyo.

Kama jina la app hii lilivyo, kupitia app hii utaweza kutengeneza video bora kwaajili ya mtandao wa Instagram pamoja na mtandao wa YouTube. Mbali na hayo app hii inakuja na sehemu nyingi za kufanya utengeneza video zako vizuri na ziwe kwenye ubora wa kipekee.

App nyingine kwenye list hii ni app ya Viva Video, App hii pia inakujulikana sana na kutumiwa na watu wengi hivyo sitopoteza muda mwingi sana kuiengelea. Kama unataka kutengeneza video bora na kwa urahisi basi jaribu app hii ya Viva Video.

App ya mwisho kwenye list hii ni Vlog it, app ni nzuri sana kwa wale wanao anza ku-edit vido bila usumbufu, app hii haina matangazo na inakuja na sehemu nyingi sana za kuedit video kwa urahisi. Mbali ya hayo pia utaweza kutengeneza picha kwaajili ya kuweka kwenye video zako wakati unataka ku-upload video hizo kupitia mtandao wa YouTube.

Na hizo ndio apps nzuri ambazo unaweza kuzitumia ku-edit video kwa ajili ya youtube kwenye simu yako ya mkononi. Kama unataka kujua app nyingine nzuri unaweza kusoma hapa kujua app nzuri ambazo zinaweza kusaidia kufanya meseji zako za WhatsApp zijitume zenyewe.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use