Apps# 5 : Jaribu App Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android

Jaribu programu hizi bora za Android kwenye simu yako sasa
Apps# 5 : Jaribu App Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android Apps# 5 : Jaribu App Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android

Kama kawaida ya Tanzania Tech tunakuletea programu bora za Android za kujaribu kwenye simu yako. Wote tunajua kuwa soko la Play Store limejaa programu nyingi mbalimbali ambazo wengi wetu hatuzijui, Tanzania Tech tumepanga kukusaidia kwenye hilo na kukuletea programu bora za kujaribu kwenye simu yako ya Android.

Basi bila kupoteza muda twend tuka angalie programu hizi tulizo kuandalia siku hii ya leo, kumbuka unaweza kudownload programu hizi kwenye simu yako kwa kubofya jina la programu husika.

1. Vyng Video Ringtones

Programu hii itakusaidia kuweza kuweka ringtone ya simu yako kuwa video, yaani badala ya kuweka ringtone ya muziki pekee, app hii itakusaidia kuweza kuweka video kama ringtone na itaonekana juu ya kioo chako pale mtu anapo kupigia.

Advertisement

2. Roomle 3D/AR Furniture Catalog

Roomle ni programu bora kwa wale watu wanaotaka kununua samani za ndani au furniture, App hii itakuwezesha kuweza kujaribu samani hizo kwenye nyumba yako kabla ya kununua. Yani unachoweza kufanya ni kuchagua aina ya samani kisha kwa kutumia kamera ya simu yako utaweza kujaribu samani hizo kama vile zipo kwenye nyumba yako.

3. Chkfake – Check Fake Money

Chkfake ni programu mpya na nzuri kutumia kama wewe unatumia pesa za kigeni mara kwa mara. App hii itakusaidia kujua noti feki za dollar pamoja na noti zingine feki za kigeni. App hii ni nzuri sana na itakusaidia sana kujua noti feki za kigeni.

4. Socratic – Math Answers & Homework Help

Socratic
Price: Free

Socratic ni programu itakayo kusaidia sana kama wewe ni mwanafunzi, app hii itakusaidia kupata majibu mbalimbali ya maswali yako ya hesabu, chemistry, Physics na masomo mengine kama historia. Unachotakiwa kufanya ni kupiga picha swali na app hii itakusaidia kujibu maswali yako kwa kuonyesha njia ya kupata jibu ikiwa pamoja na jibu lenyewe.

5. Plu.us – Your online world in one word

App hii ni moja kati ya app nzuri sana kwenye list hii, App hii itakusaidia kuweza ku-unganisha link zako zote za mitandao ya kijamii kuwa kwenye link moja. Yani kuliko kuwa na link mbalimbali ambazo huwezi kuziweka kwenye wasifu wako wa instagram app hii itakusaidia kutengeneza link moja tu kwaajili ya mitandao yako yote. Lakini cha muhimu ni kuhakikisha unawahi kujisajili ili uweze kupata link yako mapema kabla mtu ajachukua. Kuelewa zaidi angalia link hii ya Tanzania Tech Bofya Hapa.

Na hizo ndio programu nilizo kuandalia kwa siku ya leo, kama ulipitwa na list ya App zilizo pita unaweza kujaribu App hizo kwa kubofya hapa. Kwa kujua programu zaidi za Android endelea Tanzania Tech kila siku.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use