Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

App 13 za Kubadilisha Muonekano wa Simu Yako ya Android

Badilisha muonekano wa simu yako ya Android kwa kutumia app hizi
muonekano wa simu ya Android-launcher muonekano wa simu ya Android-launcher

Kubadilisha muonekano wa simu yako ni kitu cha msingi sana, wengi wetu tumekuwa tukichoka simu zetu kutokana na kubaki na muonekano wa aina moja kwa muda mrefu. Kuliona hilo leo tunakuleta programu nzuri za Android ambazo zinaweza kukusaidia kubadilisha muonekano wa simu yako na kufanya uone simu yako mpya kabisa.

Programu hizi ni nzuri sana na zote zinapatikana kupitia soko la Play Store, unaweza kupakua programu hizi kwa kubofya link ya programu husika chini ya jina la App hiyo. Basi bila kupoteza muda twende tukaangalie app hizo.

Advertisement

1. Nova Launcher

Nova Launcher
Price: Free

Wakati wowote unapotaka programu nzuri za kuweza kubadilisha muonekano wa simu yako ya Android basi Nova Launcher ni moja ya App ambayo ni lazima uweze kujaribu. App hii ni rahisi kutumia na inakupa uwezo wa kubadilisha karibia kila kutu kwenye simu yako.

2. ADW Launcher 2

ADW Launcher 2
Price: Free

App nyingine nzuri ya kuweza kukusaidia kubadilisha muonekano wa simu yako ni pamoja na app hii ya ADW Launcher 2, App hii ni nzuri sana na pia ni moja kati ya app ambazo inawezekana ni app bora kwa mwaka huu 2018.

3. Action Launcher 3

App nyingine ambayo ni bora kwaajili ya kubadilisha muonekano wa simu yako ni app ya Action Launcher 3, App hii ni nzuri sana na inakuja na sehemu nyingi ambazo zinaweza kukusaidia kubadilisha muonekano wa simu yako kwa haraka.

4. Evie Launcher

Evie Launcher
Price: Free

Evie Launcher ni app nyingine nzuri sana kwa watu wanaotaka kubadilisha muonekano wa simu zao, App hii ni rahisi sana kutumia na inafanya kazi kwa haraka zaidi pengine kuliko app nyingine kwenye list hii.

5. Apex Launcher

Apex Launcher
Price: Free

Apex Launcher ni app nyingine nzuri sana ya kubadilisha muonekano wa simu yako ya Android, App hii pia ni moja kati ya app nzuri sana inayojulikana na watu wengi.

6. ASAP Launcher

ASAP Launcher
Price: Free

Muonekano mwingine unaweza kubadilishwa kwa kutumia App ya ASAP Launcher, App hii ni nuzri sana na ni rahisi sana kutumia. App hii haina sehemu nyingi sana lakini ni moja kati ya app inayoweza kubadilisha muonekano wa simu yako kwa haraka.

7. Google Pixel Launcher

Pixel Launcher
Price: Free

Kama wewe ni mpenzi wa simu za Google Pixel basi hii ni moja ya app ambayo unaweza kujaribu kupata muonekano wa simu za Google Pixel. App hii imetengenezwa na Google hivyo inamuonekano mzuri na inafanya kazi kwa haraka zaidi.

8. Buzz Launcher

Kama unataka kutumia Theme mbalimbali ili kubadilisha muonekano wa simu yako ya Android, App ya Buzz Launcher ni app nzuri sana kwaajili yako. App hii inakupa uwezo wa kutumia theme mbalimbali kuweza kubadilisha muoenekano wa simu yako kwa haraka zaidi.

9. Launcher 8 WP style

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaopenda muonekano wa Windows kwenye simu yako basi app hii ni kwaajili yako. App hii ni nzuri sana na inakupa uwezo kuweka muonekano wa Windows 10 kwenye simu yako, unaweza kujaribu app hii na uhakika kama unapenda muonekano wa Windows utapenda pia muonekano wa app hii kwenye simu yako.

10. Smart Launcher 5

Smart Launcher 6
Price: Free

App nyingine yenye kukupa muonekano mzuri kwenye simu yako ni pamoja na app ya Smart Launcher 5, app hii inakupa urahisi wa kubadilisha karibia kila kitu kwenye simu yako ni rahisi sana kutumia na nauhakika utaipenda.

11. Microsoft Launcher

Microsoft Launcher
Price: Free

App nyingine ya kubadilisha muonekano wa simu yako ya Android ni app ya Microsoft Launcher, App hii itakupa muonekano mzuri sana na rahisi kutumia, unaweza kubadilisha kila kitu kwenye simu yako na kwa haraka kabisa. App hii inatokea Microsoft hivyo ni mmoja kati ya app zenye ubora wa kipekee.

12. Lawnchair Launcher

Lawnchair Legacy
Price: Free

Lawnchair launcher ni moja kati ya app mpya na bora ambazo zinaweza kukusaidia kubadilisha muonekano wa simu yako kwa urahisi na haraka. Japo kuwa app hii ni mpya lakini inakupa muonekena bora na rahisi sana kutumia.

13. SquareHome 2

Square Home
Price: Free

App nyingine bora ya kukusaidia kubadilisha muonekano wa simu yako ya Android ni hii ya SquareHome 2, app hii ni nzuri na ni rahis sana kutumia na inauwezo wa kukupa muonekano bora kwenye simu yako.

Na hizo ndio app nzuri za kuweza kukusaidia kubadilisha muonekano wa simu yako, App hizi kama nilivyosema hapo awali zinapatikana kupitia Play Store unaweza kuzipakua kwa kutumia link hapo chini. Kama unataka kujua app nyingine nzuri unaweza kusoma makala yetu iliyopita.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use