Aina Tatu za Telegram Bots Bora, Jaribu Kupitia Telegram

Fanya mengi zaidi kupitia app ya Telegram Android au iOS
Aina Tatu za Telegram Bots Bora, Jaribu Kupitia Telegram Aina Tatu za Telegram Bots Bora, Jaribu Kupitia Telegram

Ni wazi kuwa telegram ni moja ya programu bora za kuchati ambazo pia ni Open Source, Programu hii kuwa Open Source inasaidia mtu yoyote kuweza kutengeneza programu nyingine juu ya Telegram na kufanya app hii kurahisisha mambo mengi zaidi ya mawasiliano.

Sasa kama wewe ni mtumiaji wa Telegram ni lazima utakuwa unafahamu kuhusu Telegram bots, Kama ufahamu pengine nikueleze kwa ufupi kabisa.

Telegram bots ni programu ndogo ndogo ambazo hutengenezwa ndani ya programu ya Telegram, programu hizi kufanya kazi ndani ya Telegramu kwa kutuma maelekezo mbalimbali kupitia sehemu ya kawaida ya kuchati ndani ya app ya Telegram.

Advertisement

Aina Tatu za Telegram Bots Bora, Jaribu Kupitia Telegram

Sasa baada ya kufahamu kidogo kuhusu telegram bots basi moja kwa moja twende kwenye makala ambayo na uhakika itakusaidia kufanya mambo kwa urahisi kupitia Telegram.

Kupitia makala hii nitakuonyesha aina tatu za telegram bots ambazo zitaweza kusaidia kufanya mambo kwa urahisi na haraka, Basi bila kuendelea kupoteza muda wako zaidi twende moja kwa moja kwenye bots hizi.

Fahamu Jina la Mtu Kupitia Namba ya Simu

Kama unataka kufahamu jina la mtu yoyote kupitia namba yake ya simu basi Telegram bots hii itakusaidia kufanya hivyo kwa urahisi.

Unachotakiwa kufanya ni kutuma namba ya simu ambayo unataka kutambua jina lake na moja kwa moja bots hii itakurudishia jina la mmiliki wa namba hiyo ikiwa pamoja na barua pepe ya mmiliki.

Aina Tatu za Telegram Bots Bora, Jaribu Kupitia Telegram

Kama unavyoweza kuona hapo juu kwa kuweka namba yangu binafsi bots hii imeweza kurudisha jina langu pamoja na mtandao naotumia ikiwa pamoja na barua pepe yangu. Unaweza kujaribu bots hii kupitia link hapo chini. Kitu cha muhumi hakikisha namba ina anzia na +255 mfano +255713711233.

Jaribu Bots Hii Hapa

Tuma Meseji WhatsApp Bila Kusave Namba

Kama wewe ni mtumiaji wa WhatsApp kibiashara ni wazi kuwa umesha hitaji hii ya kutuma meseji ya WhatsApp bila ku-save namba ya mtu kwenye simu yako.

Sasa najua kuwa zipo apps nyingi zenye kufanya kazi hii lakini kama huitaji kupakua apps nyingi kwenye simu yako basi kupitia Telegram unaweza kumtumia mtu meseji bila kusave namba yake.

Unachotakuwa kufanya ni kufungua bots husika (kupitia link hapo chini) kisha tuma namba unayotaka kutumia meseji kisha moja kwa moja bost hii itakutumia link ambayo itafunguka kwenye WhatsApp na utaweza kuchat na mtu moja kwa moja bila kuhifadhi au kusave namba yake.

Aina Tatu za Telegram Bots Bora, Jaribu Kupitia Telegram

Kama unavyoweza kuona baada ya kutuma namba ya simu moja kwa moja bots hii itarudisha link yenye maneno “Open Chat” na kwa kubofya hapo moja kwa moja utaweza kuanza kuchat na mtu bila kusave namba ya mtu kwenye simu yako.

Jaribu Telegram bots hiyo hapo chini, kama ilivyo hatua za awali hakikisha pia unatuma namba ya mtu kwa kuanza na +255.

Jaribu Bots Hii Hapa

Tumia Telegram Kama File Manager (Share Files)

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao umekuwa ukishare vitu mbalimbali na watu au kama unataka kushare file lolote na mtu yoyote basi bots hii itakusaidia sana.

Unacho takiwa kufanya ni kufungua bots hii kisha chagua file ambalo unataka kushiriki na mtu yoyote na moja kwa moja bots hii itakutumia link ambayo mtu yoyote ataweza kupakua file hilo kwa urahisi na haraka.

Aina Tatu za Telegram Bots Bora, Jaribu Kupitia Telegram

Kama unavyoweza kuona hapo juu, baada ya ku-upload file moja kwa moja utaletewa link husika kama unavyo ona hapo juu, pamoja na link za kushare file hilo kwenye mitandao kama WhatsApp, Facebook na mitandao mingine. Unaweza kujaribu bots hii hapo chini.

Jaribu Bots Hii Hapa

Na hizo ndio bots nzuri ambazo unaweza kujaribu kwenye app yako ya Telegram, kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanataka kujifunza kutengeneza bots tumeandaa makala ambayo tutaiweka siku za karibuni hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Kama unalo swalo lolote ambalo unataka tukujibu kwa urahisi unaweza kuuliza kupitia Telegram Group hapa na tutaweza kujibu moja kwa moja. Unaweza kusoma hapa kujua aina nyingine za Telegramu bots nzuri kuzifahamu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use