Jinsi ya Kutengeneza Picha kwa Maandishi (Kwa Kutumia AI)

Andika maneno unayo fikiria na mfumo huu wa AI utatengeneza picha
Jinsi ya Kutengeneza Picha kwa Maandishi (Kwa Kutumia AI) Jinsi ya Kutengeneza Picha kwa Maandishi (Kwa Kutumia AI)

Ni wazi kuwa tumesha ongelea sana kuhusu mambo ya Artificial Intelligence au AI, lakini hadi sasa hatukuwahi kuongelea njia hii ambayo ni njia ya kipekee kuliko njia nyingi ambazo unazifahamu.

Kupitia makala hii nitakuonyesha njia rahisi sana ya kutengeneza picha au kubuni picha kwa kuandika jinsi unavyotaka picha hiyo ionekane na mfumo wa AI utaweza kutengeneza picha hiyo moja kwa moja.

Yani kwa mfano ukitaka mfumo huu wa AI uweze kutengeneza picha ya “Nyani akipanda mlima kilimanjaro” mfumo huu wa AI unaweza kutengeneza picha kama unavyoweza kuona hapo chini.

Advertisement

Jinsi ya Kutengeneza Picha kwa Maandishi (Kwa Kutumia AI)

Kama unavyoweza kuona mfumo huu hautoi picha kwenye tovuti yoyote bali unatengeneza picha hizi moja kwa moja kwa kutumia mfumo wa AI au Artificial Intelligence. Kitu cha muhimu ni kuandika unachotaka kiwepo kwenye picha na mfumo huu utaweza kutengeneza picha hiyo.

Basi kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanataka kubadilisha ubunifu wako wa maandishi kuwa kwenye picha moja kwa moja twende kwenye makala hii.

Hatua ya kwanza unahitaji akaunti ya Google au barua pepe yenye kufanya kazi, kisha moja kwa moja bofya link hapo chini na tengeneza akaunti yako.

Tembelea Tovuti Hapa

Jinsi ya Kutengeneza Picha kwa Maandishi (Kwa Kutumia AI)

Kama unataka kujisajili kwa haraka unaweza kutumia akaunti yako ya Google ili kuanza kutumia mfumo huu moja kwa moja.

Baada ya kujisajili, kama uli jisajili kwa kutumia barua pepe binafsi (kwa kujaza sehemu ya email) basi unatakiwa kuthibitisha barua pepe yako moja kwa moja. Angalia inbox yako na utaweza kuthibitisha barua pepe tayari kuanza kutumia mfumo huu.

Jinsi ya Kutengeneza Picha kwa Maandishi (Kwa Kutumia AI)

Baada ya kumaliza kujisajili moja kwa moja utaletwa kwenye ukurasa kama kwenye picha hapo juu na sasa unatakiwa kuandika kitu unachotaka kiwepo kwenye picha yako.

Hapa kama unataka kutumia Kiswahili moja kwa moja fungua Google translate na kisha andika kwa kiswahili kitu unachotaka na kisha nakili maelezo ya kingereza na paste kwenye sehemu hiyo.

Jinsi ya Kutengeneza Picha kwa Maandishi (Kwa Kutumia AI)

Kama hutaki kutumia website ya Google Translate unaweza kutumia app ambayo inapatika kwenye mifumo yote ya Android na iOS.

Sasa baada ya kupata maelezo unayotaka moja kwa moja bofya Generate, na subiri kidogo utaweza kuona mfumo huu ukitengeneza picha yenye maelezo uliyo andika na moja kwa moja utaweza kupakua picha unayota na kutumia sehemu yoyote unayotaka.

Kumbuka picha hizi unaweza kuzitumia kwa kuwa hazi milikiwi na mtu mwingine kwani zimetengenezwa moja kwa moja kupitia mfumo huu.

Jinsi ya Kutengeneza Picha kwa Maandishi (Kwa Kutumia AI)

Kama unavyoweza kuona utaweza kutengeneza picha kwa ubinifu wako wewe mwenyewe. Ni rahisi na unaweza kutengeneza picha zenye ubora na kudownload picha hizo moja kwa moja kwa kubofya picha usika.

That’s it! hiyo ndio njia ambayo unaweza kutumia kutengeneza picha kwa maandishi moja kwa moja kwa kutumia mfumo wa AI au Artificial Intelligence. Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu AI unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutengeneza Muziki kwa kutumia AI hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use