Fahamu Hili Kabla ya Kununua Simu Yoyote ya iPhone

Angalia kama simu yako ni Mpya, Refurbished au Replacement unit
Fahamu Hili Kabla ya Kununua Simu Yoyote ya iPhone Fahamu Hili Kabla ya Kununua Simu Yoyote ya iPhone

Kama wewe ni mtumiaji wa simu za iPhone basi makala hii ni kwa ajili yako, na pia kama unafikiria kununua simu mpya ya iPhone au hata kama unataka kununua simu used basi ni vyema umechagua kusoma makala hii.

Kupitia makala hii nitaenda kukujulisha moja kati ya jambo la muhimu sana la kuangalia kabla ya kununua au kumiliki simu mpya ya iPhone.

Kwa kuanza labda pengine unafahamu au ufahamu lakini zipo simu nyingi za iPhone zenye sifa mbalimbali, kuna simu za iPhone ambazo ni mpya kabisa yaani hazijawahi kutumika na mtu yoyote na kuna simu za iPhone ambazo ni refurbished yani zilikuwa na tatizo zikarudisha na kufanyiwa marekebisho na kurudishwa sokoni kama simu mpya.

Advertisement

Sasa pengine unaweza kudhania simu hizo zinakuja zikiwa used hapana, bali zinakuja zikiwa kwenye box lake kabisa na seal zote ziki wepo kwani simu hizi hutoka moja kwa moja Apple lakini zikiwa kama refurbished.

Jinsi ya Kujua Simu Refurbished za iPhone

Sasa ili kujua kama unanunua simu ambayo ilishawahi kutumika kwa namna yoyote hizi hapa ni hatua za muhimu za kufuata. Kama unato simu ya iPhone basi fuata hatua hizi, pia kama unataka kununua pia hatua zinafuata chini yake.

  1. Ingia Kwenye Settings Kwenye Simu yako kisha chagua General kicha About
  2. Angali kwenye Model Number
  3. Kisha Angalia Namba ya Kwanza Kwenye Model Number

Fahamu Hili Kabla ya Kununua Simu Yoyote ya iPhone

F – Herufi hii inaonyesha iPhone iliyotengenezwa tena (refurbished). Mara nyingi inaonyesha simu hiyo ilitengenezwa yaani imerudishwa kwa Apple, na kisha kutengenezwa na kurejeshwa katika hali mpya kabisa kabla ya kuuzwa tena.

M – Herufi “M” inawakilisha simu mpya ya iPhone (retail unit). Hii inaonyesha simu yako ya iPhone ni mpya kabisa na ambavyo inauzwa moja kwa moja kwa wateja kupitia wauzaji halali au maduka ya rejareja ya Apple.

N – Herufi “N,” inaonyesha kifaa cha kubadilishwa (replacement unit). Vifaa vya kubadilishwa mara nyingi hutolewa na Apple au watoa huduma walioruhusiwa kwa wateja ambao wamekutana na shida na kifaa chao cha awali na wanastahiki kupata kifaa mbadala kupitia huduma kama Apple Care.

P – Herufi “P” inaonyesha kifaa kilichobinafsishwa au kilichochorwa (Personalised). Hizi ni iPhone ambazo zimeboreshwa na uchoraji wa kibinafsi au ujumbe maalum ulioombwa na wateja wakati wa mchakato wa kuagiza.

Kujua Model Number Kabla ya Kufungua Box

Kama unataka kujua model Number Kabla ya kufungua Box angalia nyuma ya box la simu husika neno la kwanza kabisa kwenye label. Hakikisha Model number inafanan na simu pale utakapo washa, kama hifanani Herufi ya kwanza pekee basi angalia Herufi hapo juu kujua ni aina gani ya simu unayo nunua. Kumbuka mara nyingi kwenye box simu zote zina anza na herufi “M” hivyo ni vizuri kuangalia ndani kujua zaidi.

Fahamu Hili Kabla ya Kununua Simu Yoyote ya iPhone

Bila shaka hadi hadi hapo utakuwa umepata mwanga kidogo mambo ya kuangalia kabla ya kununua simu yako mpya ya iPhone.

Ni muhimu kuelewa kwamba ingawa herufi hizi zinaonyesha Model ya simu yako ya iPhone, lakini haina maana ya moja kwa moja kwamba simu yako sio mpya. Kwa maelezo zaidi unaweza kusoma zaidi kwenye tovuti ya Apple kujua zaidi.

Kama unataka kujua jinsi ya kuangalia Model number kwenye simu yako ya iPhone unaweza kutembelea hapa kujua zaidi.

1 comments
  1. Dah hapa nimepata Funzo kubwa sana hapa kuhusu simu za Iphone kwa hili wako vizuri sana. Vipi kuhusu Android hakuna hii Ili tuweze kujua??

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use