Ongeza Uwezo wa Simu Yako Kupitia Apps Hizi za Android

Kupitia apps hizi utaweza kufanya simu yako kufanya kazi kwa upekee
Ongeza Uwezo wa Simu Yako Kupitia Apps Hizi za Android Ongeza Uwezo wa Simu Yako Kupitia Apps Hizi za Android

Karibuni tena kwenye makala nyingine ya Apps nzuri za Android, kama kawaida hapa tunapata nafasi ya kuweza kuangalia Apps nzuri za android ambazo zinaweza kufanya matumizi ya simu yako ya Android kuwa rahisi.

Kama wewe ni mgeni napenda kukukaribisha sana na kama wewe ni msomaji wa makala hizi basi kumbuka unaweza kusoma makala nyingine kama hizi za app nzuri kwa kubofya link inayopatikana mwishoni mwa makala hii.

Futa Mafaili Yaliyo Jirudia

Ongeza Uwezo wa Simu Yako Kupitia Apps Hizi za Android

Advertisement

Kama kwenye simu yako kuna majina yaliyojirudia, picha, nyimbo au hata Video basi app hii itakusaidia kufuta vitu hivyo vilivyo jirudia na kuacha simu yako ikiwa na picha, majina au nyimbo za aina moja yaani ambazo hazija jirudia.

Download App Hapa

Zuai Vitu Kufutika kwa Bahati Mbaya

Ongeza Uwezo wa Simu Yako Kupitia Apps Hizi za Android

App hii ya Dumpster ni app nyingine nzuri sana kwa watumiaji wa simu za Android, App hii inakupa uwezo wa kuzuia kupoteza vitu hasa vile unavyofuta kwa bahati mbaya kwenye simu yako ya Android. Yaani kifupi ni kuwa app hii ni kama vile sehemu ya takataka au Recycle Bin kwenye kompyuta yako, pale unapo futa kitu unaweza kukipata ndani ya App hii.

Download App Hapa

Ficha Picha na Video kwa Urahisi

Ongeza Uwezo wa Simu Yako Kupitia Apps Hizi za Android

Ni kweli kwamba kila mtu anahitaji usiri kidogo kwenye simu yake, iwe huna chochote cha kuficha au hata kama una vitu vya siri ambavyo hutaki watu waweze kuviona ni wazi kwamba usiri ni lazima hasa hasa kwenye sehemu ya picha. App hii ya keepsafe ni muhimu sana kuwa nayo kwani itakupa uwezo pekee wa kuficha picha. App hii haitoficha sehemu ya Gallery bali itaficha baadhi tu ya picha ambazo utakuwa unataka zifichwe na utaweza kuzifungia kwa kutumia fingerprint au hata password.

Download App Hapa

Fanya SMS au Simu Ijipige kwa Muda Fulani

Ongeza Uwezo wa Simu Yako Kupitia Apps Hizi za Android

Hii ni app nzuri sana ambayo itakusaidia kuweza kufanya mambo mbalimbali kwenye simu yako bila kushika simu yako, unaweza kuset app hii iweze kutuma meseji kwa muda flani, pia unaweza kuset app hii ikusaidie kupiga simu kwa muda flani pamoja na kufanya mambo mengine kama kuwasha muziki kwenye simu yako na mambo mengine kama hayo.

Download App Hapa

Kumbuka Muda wa Kunywa Maji

Ongeza Uwezo wa Simu Yako Kupitia Apps Hizi za Android

Maji yana umuhimu sana mwilini, lakini wengi wetu tumekua tukiangalia simu zetu mara nyingi kuliko hata tunavyo kunywa maji. Sasa app Hii itakusaidia kukumbuka kunywa maji ikiwa pamoja na kiasi cha maji unachotakiwa kunywa kwa siku kulingana na uzito wa mwili wako. App hii nzuri sana na itakusaidia kuepukana na magonjwa mbalimbali ambayo husababishwa na ukosefu wa maji.

Download App Hapa

Fahamu Dalili za Ugonjwa Unaokusumbua

Ongeza Uwezo wa Simu Yako Kupitia Apps Hizi za Android

Tukiwa bado tuko kwenye upande huo huo wa Afya, Kama umekua ukijisikia vibaya mara kwa mara na hujui cha kufanya basi App hii ni  nzuri sana kwako. App hii itakusaidia kuweza kujua dalili za ugonjwa mbalimbali ushauri mbalimbali wa kiafya pamoja na njia mpya ya kuweza kupata ushauri wa kidaktari bure kupitia simu yako ya mkononi. Kizuri ni kuwa app hii ipo kwa kiswahili.

Download App Hapa

Fanya Mazoezi Bora Bila Kwenda Gym

Ongeza Uwezo wa Simu Yako Kupitia Apps Hizi za Android

Najua kuwa kwenye soko la Play Store kuna app nyingi sana za mazoezi, lakini app hizo nyingi hazija tengenezwa kwaajili ya watanzania wa kipato cha kawaida hiyo ni kutokana na vifaa vinavyo itajika ili kuweza kufanya mazoezi. Hilo ni tofauti kwenye app hii kwani app hii itakupa uwezo wa kufanya mazoezi ambayo hayaitaji wewe uende GYM au kuwa na vifaa vya aina yoyote. App hii itakuonyesha mazoezi ya kawaida lakini yenye nguvu ambayo yatakusaidia kupata mwili mzuri na wenye afya.

Download App Hapa

Na hizo ndio apps ambazo zinaweza kusaidia sana kuongeza uwezo wa simu yako ikiwa pamoja na kusaidia kwenye maisha yako ya kila siku. Kumbuka apps hizi zote ni muhimu na zinafanya kazi bora sana kwenye simu yako ya Android.

Kama unataka kufahamu apps nyingine nzuri zaidi unaweza kusoma hapa kujua apps nzuri ambazo unaweza kujaribu zaidi kwenye simu yako ya Android.

Kama unataka kujifunza kwa vitendo hakikisha unatembelea channel yetu ya Tanzania tech kupitia kwenye mtandao wa YouTube hapa na utajifunza mambo mbalimbali kwa vitendo. Kwa habari zaidi endelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use