in ,

Jinsi ya Kuangalia Channel Zaidi ya 5000+ Kupitia Android TV

Angalia IPTV mpya zaidi ya 5000+ kwenye Smart TV yako

Jinsi ya Kuangalia Channel Zaidi ya 5000+ Kupitia Android TV

Ni wazi kuwa kwa sasa smart TV zimekuwa zikipatikana kwa wingi sana hasa hapa Tanzania, mbali ya upatikanaji pia bei ya TV hizi pia imekuwa ni nafuu sana kutokana na wingi wa TV hizi.

Sasa kwa sababu ya hili ni wazi kuwa unaweza sasa kutumia Smart TV yako kama ilivyo simu yako ya Android, tukianza na njia hii ya jinsi ya kuangalia IPTV kupitia Smart TV yako yenye kutumia mfumo wa Android.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa kuanza kama kawaida unatakiwa ku-download app ya IPTV kupitia link hapo chini, baada ya kudownload usijali nitaenda kuonyesha hatua nyingine za muhimu unazo takiwa kufanya.

Download App Hapa

Baada ya kudownload app hii hakikisha una install kwenye TV yako, kama TV yako inayo browser unaweza kutembelea ukurasa huu kupitia TV yako na kudownload app hii moja kwa moja.

Baada ya hapo moja kwa moja tembelea ukurasa huu kisha bofya sehemu iliyo andikwa Copy Link au bofya hapo chini, kisha nakili link hiyo, kisha moja kwa moja fungua app ya IPTV kisha bofya sehemu ya Load Your Playlist or File/URL na kisha paste link hiyo kwenye sehemu hiyo.

Copy Link Hapa

Jinsi ya Kuangalia Channel Zaidi ya 5000+ Kupitia Android TV

Baada ya hapo moja kwa moja utaweza kuona channel zaidi ya 5000+ ambazo utaweza kuangalia moja kwa moja kupitia Smart TV yako ya Android. Kumbuka unatakiwa kuwa na Internet kwenye TV yako ili kuweza kuangalia channel hizi kwenye TV yako.

Kitu cha muhimu ni kuwa angalia channel hizi zipo nyingi sana kiasi kwamba sio channel zote zenye maadili hivyo hakikisha unakuwa makini unapo weka channel hizi kwenye TV yako ya sebuleni kwako, hasa kama kuna watoto.

Baada ya kusema hayo basi bila shaka umeweza kuangalia IPTV kupitia kwenye Smart TV yako, kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa jinsi ya kuzima bluetooth kwenye Smart TV yoyote inayotumia mfumo wa Android.

Code za Siri za Smartphones Mbalimbali (Njia Rahisi)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.