Kampuni ya TECNO Yazindua Rasmi Spark 10 PRO

SPARK 10 PRO ni simu ya kisasa na yenye gharama nafuu
Kampuni ya TECNO Yazindua Rasmi Spark 10 PRO Kampuni ya TECNO Yazindua Rasmi Spark 10 PRO

Kampuni ya simu za mkononi TECNO Tanzania imetambulisha rasmi toleo jipya la muendelezo wa Series ya SPARK ambayo ni TECNO SPARK 10 PRO.

TECNO SPARK 10 PRO ni simu ya kisasa na yenye gharama nafuu na sifa yake kubwa zikielekezwa kwenye uhodari wa MP32 za selfie kamera na MP 50 za kamera ya nyuma, zinang’arisha picha na kuzifanya kuwa na quality ya hali ya juu.

Advertisement

Kampuni ya TECNO Yazindua Rasmi Spark 10 PRO

“Sifa nyengine ambazo zinaifanya simu hii kuwa ya kipekee na yenye kuvutia ni wepesi wa bei ukilinganisha na unachokipata.

Pamoja ya kuwa na kamera mahiri vile vile TECNO SPARK 10 PRO inaumbo la kupendeza lenye skrini ya inch 6.78FHD, RAM ya GB8 inaongezeka hadi GB16, ROM ya GB256, toleo jipya la Android 13, processor G88 pamoja na warranty ya miezi 13”, alisema hivyo Bi Shakira Mkima Mkufunzi wa simu za TECNO Tanzania.

Kampuni ya TECNO Yazindua Rasmi Spark 10 PRO

Katika kuikaribisha simu hii sokoni TECNO Tanzania imeshirikiana kwa ukaribu na Kampuni ya Mawasiliano Tigo Tanzania.

Akizungumza na vyombo vya habari Imeld Edward, Meneja wa Vifaa Tigo alisema, “Uhusiano wa kuaminika tulionao na Kampuni ya sim TECNO unamchango mkubwa katika kuwapa wateja wetu vifaa bora zaidi.

TECNO SPARK 10 PRO itafungua uwezo kwa wateja wengi zaidi kupata huduma zetu kupitia mtandao wetu wa 4G lengo letu ni moja kukuza maisha ya kidijitali nchini Tanzania na kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma hivyo basi tunatoa ofa ya GB78 za internet BURE kwa wateja wa TECNO SPARK 10 PRO”.

Kampuni ya TECNO Yazindua Rasmi Spark 10 PRO

TECNO SPARK 10 PRO inapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use