in

Jaribu Leo App Hizi Kwenye Simu Yako ya Android

Badilisha matumizi ya simu yako kupitia app hizi za Android

Jaribu Leo App Hizi Kwenye Simu Yako ya Android

Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Android basi ni wazi kuwa unajua kuwa apps ndio zinafanya simu yako kuwa smart, kuliona hili leo tumekuetea app nzuri ambazo zinaweza kusaidia kutumia simu yako kwa namna ya kipekee.

Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja tukangalie app hizi nzuri ambazo unaweza kujaribu kwenye simu yako ya Android. Kumbuka unaweza kupakua app hizi kupitia link chini ya maelezo ya app.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
Skip Ads
Price: Free

Skip Ads kama ililivyo jina lake, app hii itakusaidia sana kuweza kurusha matangazo yanayokuwa kwenye video za YouTube bila kushika simu yako. Yani kwa kupakua app hii na ku-install app utaweza kurusha matangazo ya YouTube kwa urahisi na haraka.

Download App Hapa

Jaribu Leo App Hizi Kwenye Simu Yako ya Android

Tanzania Tech ni app official ya Tanzania tech, kama ulikuwa unataka kupata makala hizi moja kwa moja kwenye simu yako ya Android kwa urahisi basi pakua sasa app ya Tanzania Tech kupitia simu yako ya Android. Hakikisha una tupa nyota 5 kama utapenda app hii.

Download App Hapa

Kama kwa namna yoyote unataka kufuta app zaidi ya moja kwenye simu yako ya Android kwa pamoja basi app hii itakusaidia sana. App hii itakupa urahisi wa kufuta app nyingi kwa pamoja na hii kukupa urahisi kuliko kutumia njia ya kuondoa app moja baada ya nyingine.

Download App Hapa

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao unataka kudownload picha, video, Stories, Reels, IGTV pamoa na profile picture za watu mbalimbali kwenye mtandao wa Instagram basi app ya Instander ni app muhimu kuwa nayo kwenye simu yako.

App hii inafanana kabisa na Instagram na unaweza kuitumia kama Instagram lakini hii itakuruhusu kudownload kitu chochote kwenye mtandao huo. Kumbuka app hii haipatikani kwenye soko la Play Store hivyo unaweza kupakua apk hapo chini.

Download App Hapa

Gazeti - Tanzania
Price: Free

Gazeti app ni app nzuri nyingine ambayo itakusaidia kupata habari zote za michezo, magazeti ya leo, habari za kimataifa, kitaifa na habari za udaku kutoka kwenye mitandao ya kijamii.

App hii ni app bora ya habari na ukiwa na app hii huna haja ya kuwa na app nyingine ya habari. Pia utaweza kupata habari kutoka kwenye kurasa maarufu kama Mange kimambi, Millard ayo na kurasa nyingine za habari na udaku.

Download App Hapa

Na hizo ndio app ambazo tumekuandalia kwa siku ya leo, kama unataka kujua app nyingine nzuri unaweza kusoma hapa kujua apps nzuri ambazo unaweza kujaribu mwezi huu April.

Kwa habari zaidi za teknolojia na maujana, hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku kwa sasa tumerudi upya.!

Amani Joseph

Jaribu Leo App Hizi Kwenye Simu Yako ya Android

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

OpenAI Mbioni Kuingiza Takribani Dola Bilioni 1 Kwa Miezi 12

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.