in

Zima na Washa Simu Kwa Kuweka Mkono Juu ya Simu

Pia utaweza kupokea simu yako kwa kuweka simu masikioni bila kubonyeza kitufe chochote

Zima na Washa Simu Kwa Kuweka Mkono Juu ya Simu0:14

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatafuta njia rahisi zaidi ya kuzima na kuwasha simu yako bila kutumia sehemu ya kuzima na kuwasha ambayo mara nyingi huwa pembeni ya simu yako basi makala hii ni kwaajili yako.

Kupitia makala hii nitakuonyesha njia rahisi ambayo utaweza kuzima na kuwasha simu yako kwa kuweka mkono juu ya simu yako ili kuzima au kuwasha simu yako. Kumbuka njia hii inafanyakazi kwa watumiaji wa simu za Android hivyo kama unayo simu ya Android basi endelea kwenye hatua zifuatazo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa kuanza moja kwa moja pakua app kupitia link hapo chini, kisha baada ya kudownload app hiyo install kwenye simu yako moja kwa moja. Baada ya hapo endelea kwa kufuata maelezo hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya kudownload app hii fungua app hii kisha bofya switch ya Enable iliyopo juu kabisa upande wa kulia.

Zima na Washa Simu Kwa Kuweka Mkono Juu ya Simu

Baada ya hapo moja kwa moja bofya sehemu kama unataka kupokea simu yako kwa kupeka mkono juu ya simu yako bila kubonyeza sehemu ya kupokea kwenye simu yako basi unaweza kuwasha sehemu hii lakini kama huitaji hiyo unaweza kuachana na sehemu hiyo kwa kubofya sehemu ya Ignore.

Zima na Washa Simu Kwa Kuweka Mkono Juu ya Simu

Kama unahitaji sehemu hiyo basi bofya sehemu ya Request na kisha bofya allow kuruhusu app hiyo kuweza kukusaidia kupokea simu kwa kuweka mkono juu ya simu yako.

Baada ya hapo moja kwa moja shuka chini kidogo ya ukurasa huo na bofya switch kwenye sehemu ya Lock screen.

Zima na Washa Simu Kwa Kuweka Mkono Juu ya Simu

Baada ya hapo unatakiwa kuwasha app hii kupitia sehemu ya Admin, bofya OK kwenye ujumbe unaotokea kwenye kioo cha simu yako na moja kwa moja utapelekwa kwenye sehemu ya Admin.

Zima na Washa Simu Kwa Kuweka Mkono Juu ya Simu

Moja kwa moja kwenye sehemu ya Admin washa app hii kwa kubofya sehemu ya Activate inayopatikana chini upande wa kulia.

Zima na Washa Simu Kwa Kuweka Mkono Juu ya Simu

Baada ya hapo utarudishwa kwenye ukurasa wa kwanza wa app hii, moja kwa moja bofya sehemu ya Lock screen kwa mara nyingine kuweza kuwasha sehemu hiyo.

Zima na Washa Simu Kwa Kuweka Mkono Juu ya Simu

Baada ya hapo moja kwa moja utakuwa uko tayari kuweza kuzima na kuwasha simu yako kwa kuweka mkono juu ya kioo cha simu yako. Ili kujaribu sehemu hii weka mkono au kiganja cha mkono wako juu kabisa karibia na kamera ya mbele ya simu yako na utaweza kuona simu yako imezima au imejiweka lock. Pia ukiweka tena mkono kwenye sehemu hiyo utaweza kuona simu yako imewaka kwa mara nyingine tena.

Kama uliwasha sehemu ya kupokea simu basi utaweza kupokea simu kwa namna ya kipekee, kwani kila mara simu yako inapo ita unaweza kuweka kwenye masikio moja kwa moja na yenyewe itaweza kupokea bila wewe kuangaika kubofya kwenye kioo cha simu yako ili kupokea.

Jinsi ya Ku-Uninstall (Kufuata App Hii)

Kutokana na app hii kutumia sehemu ya Admin, hutoweza kuondoa app hii kwa njia ya kawaida bali unachotakiwa kufanya ni kuingia kwenye app hii na moja kwa moja na ndani ya app hii slide app hii hadi mwisho na utaona sehemu ya kufuta app hii.

Zima na Washa Simu Kwa Kuweka Mkono Juu ya Simu

Kwa kufanya hivyo utakuwa umeweza kuzima na kuwasha simu yako kwa urahisi kwa kuweka mkono wako juu ya simu. Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kupokea simu na kukata bila kushika simu yako.

Fahamu Hili Kabla ya Kununua Simu Yoyote ya iPhone

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.