in

Jinsi ya Kutuma Meseji Zinazojifuta Kupitia Facebook Messenger

Tuma meseji ambazo zinafutika baada ya muda uliochagua

Jinsi ya Kutuma Meseji Zinazojifuta Kupitia Facebook Messenger

Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Facebook basi habari njema kwako, leo tutaenda kuangalia njia ya kuweza kutuma meseji zinazojifuta baada ya muda fulani kupitia app ya Facebook Messenger.

Njia hii ni rahisi na inaweza kufanya kazi kama unatumia app ya Facebook Messenger, kitu cha muhimu hakikisha una update app hiyo kupitia soko lako husika Play Store au App Store, kitu kingine cha muhimu akikisha unatumia app ya Messenger na sio Messenger Lite.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa kuanza ingia kwenye jina la mtu ambaye unataka kuchat naye kwenye app ya Facebook Messenger, kisha baada ya hapo bofya sehemu iliyo andikwa ‘Go to Secret Conversation.’

Jinsi ya Kutuma Meseji Zinazojifuta Kupitia Facebook Messenger

Baada ya hapo ukurasa mpya utafunguka wenye sehemu ya kuchat, sasa endelea kwa kuandika meseji kwenye sehemu hiyo ya kuchat kisha bofya kitufe cha saa kilichopo upande wa kushoto pembeni ya kibox cha kuchat.

Jinsi ya Kutuma Meseji Zinazojifuta Kupitia Facebook Messenger

Baada ya hapo endelea kwa kuchagua muda ambao ungependa meseji iweze kupote, baada ya kuseti muda kila meseji uliyo andika itakaa kwa muda ulio uchagua na itajifuta yenyewe.

Jinsi ya Kutuma Meseji Zinazojifuta Kupitia Facebook Messenger

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, utaweza kuruhusu meseji kudumu kuanzia sekunde tano na kuendelea, meseji zote zilizofutwa zitakuwa na alama nyeusi hivyo hazitoweza kusomeka kwa mtu yoyote.

Jinsi ya Kutuma Meseji Zinazojifuta Kupitia Facebook Messenger

Na hiyo ndio njia rahisi ambayo unaweza kuitumia kutuma meseji zinazo jifuta kupitia app ya Facebook Messenger. Kama unataka kujifunza jinsi ya kutuma meseji zinazo jifuta kupitia telegram unaweza kusoma hapa. Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku kujifunza mambo mengi zaidi, pia hakikisha unatembelea YouTube Channel yetu kuweza kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo.

Mambo Ambayo ni Adui wa Battery ya Smartphone Yako

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.