in

Jifunze Jinsi ya Kutengeneza Picha za 3D (Android)

Tengeneza picha zenye uwezo wa kusogea kushoto na kulia

Jifunze Jinsi ya Kutengeneza Picha za 3D (Android)

Kama wewe ni mfuatiliaji wa mtandao kama Facebook najua utakuwa umeshwa wahi kuona picha za 3D, picha hizi huwa zina uwezo wa kusogea kushoto au kulia, au juu au chini kadri unavyokuwa unasogeza post yoyote kwenda juu au chini.

SQUAAAARK! New 3D models on Facebook, you say? Yes please! ???? Have a play by dragging the below around with your finger or mouse.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Posted by LEGO on Tuesday, February 20, 2018

Kama unavyoweza kuona kwenye picha ya 3D hapo juu, utaweza kuzungusha picha hiyo kwa pande tatu ikiwa pamoja na juu na chini. Sasa je ungependa kutengeneza picha zako za kawaida zenye uwezo wa kusokea kama picha hiyo hapo juu.?

Kama jibu ni ndio basi moja kwa moja uko mahali sahihi kwani leo nitakuonyesha jinsi ya kutengeneza post za mtindo huo ambazo unaweza kutumia kwenye mtandao wa Facebook pamoja na sehemu nyingine mbalimbali. Mbali na hayo pia picha hizi za 3D huweza kubadilika pale unapo laza simu yako kulalia kushoto au kulia.

Basi baada ya kusema hayo, moja kwa moja twende tukangalie jinsi ya kutengeneza picha za 3D kama hiyo hapo juu moja kwa moja kwa kutumia simu yako ya Android. Kwa kuanza unatakiwa kudownload app inaitwa Phogy 3D, app hii inapatikana Play Store na unaweza kuipata kupitia link hapo chini.

Phogy, 3D Camera
Price: Free

Baada ya kupakua app hii kwenye simu yako basi moja kwa moja endelea kwa kufungua app hiyo kisha fuata maelezo mafupi ambayo yanatokea kwenye kioo cha simu yako. Unachotakiwa kufanya ni kuwasha app hii kisha bofya Skip kama ni mara yako ya pili kufungua app hii kisha chagua sehemu ya kamera na bofya sehemu ya kati ya kamera alafu zungusha simu yako kwenda upande mmoja.

Unaweza kushare picha hizo kwenye mitandao yako ya kijamii kama vile facebook, Instagram pamoja na mitandao mingine kama YouTube ambapo unaweza kuweka picha hizo zikiwa kama MP4. Hadi hapo natumaini umeweza kutengeneza picha za 3D kwa kutumia simu yako ya Android.

Kama unataka maujanja zaidi unaweza kujifunza hapa, jinsi ya kupata mawasiliano sehemu ambayo haina Network. Njia hizi ni nzuri sana kama wewe ni mtu wa kusafiri au kama bado uko kijijini kwa ajili ya likizo za sikukuu.

Amani Joseph

Jifunze Jinsi ya Kutengeneza Picha za 3D (Android)

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kuondoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments

  1. boresheni kwa kuonesha mtiririko mzuri wapicha wakati mnaonesha ufafanuzi wa hoja zenu mfano jinsi ya kuwasha tochi kwa kutikisa simu yako inatakiwa mnaonesha mtiririko na mpangilio mzuri kua unaanzia hapa unaenda hapa kwa kutumia video fupi za maelekezo au picha