in

WhatsApp Kuja na Aina Mpya ya Meseji Zinazojifuta Zenyewe

Hivi karibuni utaweza kumtumia meseji mtu bila kuwa na ushahidi

WhatsApp Kuja na Aina Mpya ya Meseji Zinazojifuta Zenyewe

WhatsApp imekuwa ikifanyiwa maboresho mapya kila mara, hivi karibuni maboresho ambayo yanatarajiwa kuja kwenye programu hiyo inayomilikiwa na Facebook ni pamoja na aina mpya ya meseji ambazo hufutika zenyewe baada ya kipindi cha muda maalumu.

Kwa mujibu wa tovuti ya WABetainfo, sehemu hiyo kwa sasa ipo kwenye programu ya majaribio ya WhatsApp Beta ambayo inapatikana kwa baadhi ya watumiaji wa Android na iOS.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa mujibu wa tovuti hiyo, ili kutumia sehemu hiyo inakubidi kuwasha sehemu hiyo wakati unachati kwa kuchagua sehemu ya info na kisha kuseti muda maalum ambao ungependa meseji hizo zijifute zenyewe. Hata hivyo utofauti wa sehemu hiyo na sehemu ya delete for everyone, sehemu hiyo haito acha ujumbe wa kujilisha meseji imefutwa bali meseji itafutika bila kuonyesha kama ili kwepo awali.

Kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu, inasemekana sehemu hiyo kwa sasa itakuwa kwenye chat za magroup, lakini pia kuna tetesi za kuwa sehemu hiyo itapatikana pia kwenye chati za kawaida ingawa hii bado haina uhakika.

Sehemu hii ya Disappearing Messages, itawasaidia sana wale watu wanaotaka kutumia meseji za siri kwa watu mbalimbali, meseji ambazo hautaki mtu awe na ushahidi nazo mara baada ya kutuma meseji hizo. Hata hivyo kwa sasa sehemu hii ipo kwenye hatua za awali za majaribio hivyo bado hakuna tarehe kamili ya lini sehemu hii ita wafikia watumiaji wote wa programu za kawaida za WhatsApp.

Kwa habari zaidi kuhusu sehemu hii pamoja na habari nyingine za teknolojia, hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku.

Ongeza Uwezo wa Simu Yako Kupitia Apps Hizi za Android

Written by Jackline John

Jack ni mpenzi wa teknolojia napenda kuandika kuhusu maujanja, simu na kompyuta. Unaweza kunipa maujanja kupitia jackline@tanzaniatech.one

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment