in

Jinsi ya Kuweka Slow Motion Kwenye Video Yoyote (Android)

Jinsi ya kurekodi video za slow mo kwenye simu yoyote ya Android

Jinsi ya Kuweka Slow Motion Kwenye Video Yoyote (Android)

Kama wewe ni mmoja kati ya watu wanaopenda kurekodi video za Slow Mo lakini huna simu yenye kamera yenye uwezo wa kurekodi video za mtindo huo basi makala hii ni kwa ajili yako. Kupitia hapa tutaenda kuangalia njia rahisi ambayo inaweza kusuidia kurekodi video kama hiyo hapo chini kupitia simu yako ya mkononi ya Android.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Video hiyo imechukuliwa na simu mpya ya iPhone 11 ambayo inakuja na uwezo wa kurekodi video za Slow-Mo kwa kutumia kamera ya selfie. Kama unataka kujua zaidi kuhusu simu hiyo mpya basi unaweza kusoma makala iliyopita hapa. Lakini kama unataka kujua jinsi ya kurekodi video za namna hii kwenye simu yako ya Android basi endelea kusoma makala hii.

Kwa kuanza unatakiwa kudownload app inayoitwa Slow motion video FX, app hii inapatikana kupitia soko la Play Store pia unaweza kudownload app hiyo kupitia link hapo chini. Bofya hapo chini na utapelekwa kwenye soko la Play Store kwa ajili ya kupakua app hii.

Baada ya kudownload app hii fungua app hii kisha utakutana na muonekano kama huo hapo chini. Bofya sehemu ya Slow Motion FX kisha chagua sehemu ya Record Movie au Choose Movie.

Jinsi ya Kuweka Slow Motion Kwenye Video Yoyote (Android)

Baada ya kuchagua video sasa chagua sehemu ya video ambayo unataka iwe kwenye Slow-Mo, kisha baada ya hapo bofya kitufe cha Start kilichopo katikati kabisa ya ukurasa huo.

Jinsi ya Kuweka Slow Motion Kwenye Video Yoyote (Android)

Baada ya hapo sasa unaweza kuchagua speed ambayo unataka video yako iwe, unaweza kuacha sehemu hiyo bila kugusa kitu pia unaweza kuweka nyimbo au sauti yoyote pamoja na filter mbalimbali. Baada ya hapo malizia kwa kubofya sehemu ya Start Processing.

Jinsi ya Kuweka Slow Motion Kwenye Video Yoyote (Android)

Baada ya hapo subiri video yako itakapo maliza utaona ipo kwenye mfumo wa Slow-Mo, App hii ina uwezo mkubwa sana wa kutengeneza video za Slow Motion kuliko app nyingine ambazo zipo kwenye soko la Play Store. Unaweza kujaribu app nyingine yenye slow mo ambayo ni rahisi kutumia ambayo inaweza kusogeleana na app hii.

Hadi hapo natumaini kuwa hadi sasa umeweza kutengeneza video za Slow-Mo, moja kwa moja kwa kupitia simu yako ya Android. Kama kuna mahali umekwama unaweza kuuliza kupia sehemu ya maoni hapo chini, kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku

Rahisisha Matumizi ya Windows Kupitia "GodMode"

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment