in

Kampuni ya TALA Yasitisha Huduma Zake kwa Nchini Tanzania

Kampuni ya Tala imatangaza kusitisha huduma za mikopo kwa Tanzania

Kampuni ya TALA Yasitisha Huduma Zake kwa Nchini Tanzania

Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni kutoka tovuti ya mwananchi, inasemekana kuwa kampuni ya TALA ambayo inajihusisha na utoaji wa mikopo ya haraka kupitia simu za mkononi, imetangaza kusitisha huduma zake kwa hapa nchini Tanzania.

Sehemu ya ripoti hiyo iliyo chapishwa kwenye akaunti ya Tala kwenye mtandao wa kijamii wa facebook inasema kuwa, “Tunakujulisha kuwa kwa sasa TALA  haitoi mikopo nchini Tanzania. Tunathamini nafasi ya kukutumikia na tunatamani wateja wetu waaminifu waendelee na mafanikio katika safari yao ya kifedha, “inasomeka taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Tunasikitika kukutaarifu ya kwamba Tala kwa sasa haitatoa mikopo Tanzania. Tunashukuru kwa kutupa nafasi ya kukuhudumia…

Posted by Tala Tanzania on Thursday, September 5, 2019

Akizungumza na Mwananchi kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Facebook, mmoja wa maofisa wa kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Kelly amesema, “Ndio, hatujatoa mikopo tena nchini Tanzania. Kwa bahati mbaya, kwa sababu za kisheria hatuwezi kusambaza habari nyingine yoyote isipokuwa ile iliyosambazwa kwenye mtandao wa kijamii.”

Kwa sasa bado hakuna ripoti zaidi juu ya hili hivyo hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech tutakupa taarifa zaidi kuhusu hili.

Amani Joseph

Kampuni ya TALA Yasitisha Huduma Zake kwa Nchini Tanzania

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment