in

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Haya ndio mambo ya msingi kwenye simu mpya ya TECNO Phantom 9

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Wiki chache zilizopita kampuni ya TECNO ilizindua simu mpya ya Phantom 9 hapa Tanzania, kama unavyojua matoleo ya simu za Phantom ni matoleo ambayo mara nyingi huwa na kila kitu ambacho pengine mtumiaji wa smartphone anakuwa anahitaji, lakini mwaka huu 2019 mambo ni tofauti kidogo sababu ni kama zifuatazo.

Kwa muda sasa nimekuwa nikitumia simu hii na baada ya wiki mbili sasa nimeona sio vibaya kushare na wewe maoni yangu kuhusu simu hii. Kupitia makala hii tutaenda kuangalia simu hii mwanzo mwisho na pia nitakwambia kwanini nadhani simu hii mpya ya TECNO Phantom 9 ni simu ya tofauti kuliko simu nyingi za TECNO zilizotoka mwaka huu 2019.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Yaliyomo Ndani ya Box

Kwanza kabla ya kuangalia vitu vingine hebu tuanze na box la Phantom 9. Kwa mwaka huu TECNO imefanya mabadiliko makubwa ya simu ya Phantom 9 na mabadiliko hayo yana anzia kwenye box la simu hii. Box hili sasa linakuja likiwa na muundo mzuri na utofauti kidogo na ukweli kwa kuangalia tu box hilo moja kwa moja unapata hisia ya simu iliyopo ndani.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Sasa mbali na box lenyewe, hebu tungalie yaliyomo ndani ya box hilo. Kwa kuanza box hilo ukifungua kwa juu unakutana na kitabu cha maelekezo ya matumizi a.k.a user manual, kitabu hicho kime ambatana na pini ya kutolea laini.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Najua unajua yote hayo yanayo kwepo kwenye box la simu, lakini sasa kitu ambacho nataka ufahamu zaidi kwenye box la Phantom 9 ni kava linalokuja na simu hii. Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanategemea kununua simu hii basi nakuahidi hutotaka kununua kava lingine la kulinda simu hii kwani kava hili linaonekana vizuri sana kwenye simu hiyo na pia ni kava gumu na bora sana kwenye simu hii ya Phantom 9 na ukweli lina feel vizuri sana.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Mengine yaliyopo ndani ya box hili ni pamoja na earphones ambazo ni nyeusi ambazo hizi ni tofauti na earphones nyingi ambazo unaweza kupata kwenye simu za TECNO za siku hizi.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Pia unakutana na waya wenye uwezo wa kuchaji simu hii pamoja na uwezo wa kuamisha data kupitia kompyuta, waya huo pia unakuja na kichwa cha kuchomeka waya huo ambacho ni cha rangi nyeupe ambacho ndio kinatumika kuchaji simu hii.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Kichwa hichi hakina teknolojia ya fast charge ila kina uwezo wa kuchaji simu yako kwa haraka ndani ya lisaa limoja au moja na nusu unaweza kuchaji simu yako ikajaa kwa asilimia 100 kwa kutumia chaji hii.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Muundo wa TECNO Phantom 9

Sasa baada ya kuangalia box hebu twende moja kwa moja tukangalie muundo wa simu hii. Kabla ujafungua kibisa simu hii, utaweza kuona inakuja na plastiki ambayo inakueleza yote ya muhimu kuhusu Phantom 9, ikiwa pamoja na sifa za awali za simu hii. Kama unavyo weza kuona kwenye picha hapo chini simu hii inakuja na kamera tatu kwa nyuma zenye mfumo wa AI, Sehemu ya fingerprint iliyopo juu ya kioo, pamoja na GB 128 za ROM na GB 6 za RAM.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Baada ya kufungua simu hii kwa nyuma Phantom 9 inakuja na rangi nzuri sana ya aurora ambayo inafanya simu hii kuwa na muonekano mzuri sana, muonekano ambao lazima watu watakuangalia pale unapo kuona unatumia simu mbele za watu wengi.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Kwa mbele simu hii inakuja na kamera nzuri sana ya Megapixel 32 ambayo ina uwezo wa kuchukua picha pamoja na video za hadi pixel 1080p. Kwa juu ya kamera hiyo kuna spika ya kusikiliza unapo pigiwa simu ambayo imejificha vizuri sana tofauti na simu nyingi za TECNO zilizo tangaulia.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Vilevile simu hii inakuja na flash mbili za LED ambazo nazo pia zimejficha vizuri sana kwa upande wa kushoto na kulia. Kwa kuangalia picha hapo juu, unaweza usijue kama simu hii inakuja na flash kwa mbele lakini ukiangalia picha hapo chini unaweza kuona uwezo mkubwa sana wa flash hizo za Phantom 9 na ukweli kwa kutumia flash hizi basi lazima picha zako za selfie zitakuwa bora na tofauti kabisa na watumiaji wa simu nyingine.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Pamoja na kuwa na vitu vyote hivi, bado simu hii mpya ya Phantom 9 imeweza kuwa na muundo mwembamba ambao kwa upande wa vipimo simu hii inakuja na unene wa milimita 7.8 tu.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Kwa upande wa kioo simu hii inakuja na kioo kikubwa na kizuri sana cha AMOLED ambacho hichi ni cha kwanza kuwepo kwenye simu ya Phantom. Sasa nadhani utakuwa hujui sana kuhusu teknolojia hizi za vioo lakini labda ni kwambie tu AMOLED ni aina ya teknolojia ya vioo vya OLED ambapo hii hufanya rangi kuwa bora na angavu zaidi. Kwa mujibu wa Techradar, vioo vya AMOLED vina uwezo wa kupitisha picha kwa haraka zaidi mara 1000 zaidi ya vioo vya LCD.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Pia kupitia kioo hicho wapenzi wa game hapa utaweza ku-enjoy game kwenye kioo kikubwa na utaweza kucheza game zaikiwa zinafanya kazi vizuri sana kwani simu hii inakuja na graphics bora ya PowerVR GE8320 ambayo kwa mujibu wa benchmark ni graphic bora kwa ajili ya game.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Eye Care na Read Mode

Kwa sababu tumetoka kuongelea maswala ya graphics hebu tuongelee swala lingine linalo husu kioo. Simu hii mpya ya Phantom 9 inakuja na mfumo maalum kwa ajili ya kulinda macho yako mfumo ambao unaweza kusaidia afya ya macho yako dhidi ya mwanga wa blue unao tengenezwa na vifaa vyote vya kielektroniki vinavyo tumia kioo. Eye care ni sehemu ambayo itakusaidia sana kuondoa mwanga huo wa blue unapo tumia simu yako hasa wakati wa usiku, pia sehemu nyingine ya Read Mode itakusaidia kuweza kusoma maandishi kwa urahisi bila kuumiza macho yako kutokana na mwanga.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Fingerprint na Face Unlock

Vile vile hatuwezi kuongelea kioo cha Phantom 9 bila kuongelea aina mpya ya Fingerprint iliyopo juu ya kioo cha simu hii. Kwa sababu ya teknolojia ya kioo cha AMOLED sasa simu hii inaweza kufunguliwa kwa urahisi kwa kutumia Fingerprint iliyopo juu ya kioo.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Mbali ya Fingerprint Phantom 9 imeongezewa ulinzi wa Face Unlock, ulinzi ambao ukweli unafanya kazi kwa haraka sana pengine kuliko simu nyingine za TECNO zenye sehemu ya Face Unlock unazo zijua wewe.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Battery na WhatsApp Mode

Kwa upande wa battery Phantom 9 inakuja na battery kubwa ya 3500 mAh battery yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa muda wa siku moja nzima kulingana na matumizi yako. Lakini kama unaona matumizi yako ni makubwa Phantom 9 inakuja na WhatsApp Mode sehemu inayo kuruhusu kutumia simu yako kwa muda mrefu zaidi bila simu yako kuisha chaji kwa haraka.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Sehemu hii husaidia app ambazo unafungua pekee ndio ziweze kutumia data na hii husaidia kuzuia kuisha kwa chaji pamoja na data kwani wote tunajua chaji huisha haraka pale simu inapokuwa inatumika zaidi.

Kamera za Nyuma

Sasa hapa ni vyema ukae vizuri kwani na uhakika utaipenda sana Phantom 9 baada ya kusikia ninacho kwambia. Kama kawaida simu hii inakuja na kamera tatu, kamera moja ikiwa inakuja na Megapixel 2 ambayo hii ni depth sensor. Kazi ya depth sensor hii ina sensor ya monochrome CMOS na projekta ya infrared ambayo husaidia kuunda picha za 3D pale unapo piga picha. Pia hupima umbali wa kila kitu unachopiga picha kwa kupeleka mwangaza usioonekana wa infrared na kupima “kiasi cha mwangaza” baada ya kamera kumulika kitu unachotaka kupiga picha.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Kamera ya pili inakuja na Megapixel 16 ambayo hii ni Main camera au kamera kuu, kazi ya kamera kuu ni kukusanya pixel zote zinazotolewa na kamera nyingine ikiwa pamoja na kamera yenyewe kuu, pia kamera hii ndio inatumika kurekebisha na kuchukua picha halisi ndio maana mara nyingi hua inakuja na pixel nyingi kuliko kamera nyingine.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Kamera ya mwisho inakuja na Megapixel 8 ambayo hii ni wide angle lens, ambayo hii inasaidia sana pale unapotaka kupiga picha ambazo unataka kuchukua eneo kubwa kwa upana. Phantom 9 imeweza sana kufanikisha hili kwani kupitia simu hii utaweza kupiga picha za upana mkubwa sana.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Kupitia kamera hizi zote utaweza kurekodi video na kupiga picha hadi za 1080p, pia utaweza kurekodi video zako kwa kutumia teknolojia ya HDR, teknolojia inayofanya video zako kuwa angavu sana na zenye rangi bora. Kama wewe ni mmoja wa watu wanaotaka kuanzisha YouTube channel basi huna haja ya kununua kamera kama utakuwa na simu hii ya TECNO Phantom 9.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Kamera hizi pia zina wezeshwa na teknolojia za Face Beautification, HDR+ scene recognition, AI FaceID, bila kusahau flash ya Dual-LED ambayo inafanya picha kuwa na mwanga bora sana hasa sehemu zenye mwanga mdogo.

Kamera ya Mbele

Phantom 9 ni simu bora lakini pia ni simu bora sana kwenye upande wa kamera, kama wewe ni mpenzi wa Selfie basi kwa Phantom 9 ndio nyumbani. Simu hii inakuja na kamera ya Selfie ya Megapixel 32, kamera ambayo inakuja na uwezo mkubwa wa kuchukua picha na video zenye muonekano mzuri sana. Kamera hii inakuja na teknolojia ya AI ambayo inafanya picha zako kuwa bora na tofauti na simu nyingine.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9

Kamera hii pia inakuja na teknolojia mbalimbali zaidi ya AI, kwani pia kuna teknolojia kama vile AR Short, Wide Selfie, Portrait, Beauty, Boken pamoja na Video Mode.

Na hayo ndio machache unayotakiwa kujua kuhusu simu hii mpya ya TECNO Phantom 9, kama unataka kujua sifa kamili za simu hii unaweza kusoma hapa. Kujua zaidi kuhusu simu hii hakikisha una subscribe kwenye channel yetu kwani siku sio nyingi tutakuwa na video ya uchambuzi mzima kuhusu simu hii. Pia kama unataka kujua mahali una-poweza kununua simu hii kwa bei nafuu basi tembelea Maduka ya Tigo Tanzania au Maduka ya TECNO Smart Hub yalito karibu na wewe au tembelea tovuti ya TECNO kwa ajili ya kupata maelezo zaidi.

Mambo Yote Usiyoyajua Kuhusu Simu Mpya ya TECNO Phantom 9
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

6 Comments