Jinsi ya Kujua Password ya WiFi Yoyote (Kwa Kutumia Simu)

Kama unataka kujua password ya Wifi iliyopotea soma hapa
jinsi ya kujua password ya wifi yoyote jinsi ya kujua password ya wifi yoyote

Kipindi cha nyuma nilishawahi kupata maoni ili niweze kusaidia kampuni moja changa ambayo ilikuwa inataka kuwezesha huduma ya WiFi kwenye eneo fulani hapa Tanzania, Lakini baada ya muda kidogo nilipata tena maoni niweze kusaidia kampuni hiyo jinsi ya kutambua password za Wifi ambazo zilikuwa zimewekwa kwa bahati mbaya na mfanyakazi wa zamani wa sehemu hiyo.

Zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo nilitumia kuweza kupata password ya WiFi hiyo na labda pengine na wewe maujanja haya yanaweza kukusaidia kupata password ya kifaa chako cha WiFi ambacho umeisahau password yake kwa namna moja ama nyingine.

KUMBUKA : Njia hii ni kwaajili ya elimu hivyo hakikisha hutumii njia hii vibaya kwa namna yoyote ile, Kumbuka nia ni kuelimishana na kusaidiana kwenye matatizo ya kiteknolojia yanayotokea kila siku na sio vinginevyo. Baada ya kusema hayo basi twende tukangalie njia hii.

Advertisement

Kwa Kutumia App ya Wifi Wps Wpa Tester

Kama kwa namna yoyote ile umesahau password yako ya WiFi, kwa kutumia app ya Wifi Wps Wpa Tester utaweza kupata password yako. Njia hii inahusisha simu ya Android na ni moja kati ya njia rahisi kwenye list hii. Unachotakiwa kufanya ni kudownload app ya Wifi Wps Wpa Tester kwa kubofya hapo chini, kisha endelea kufuata maelekezo zaidi hapo chini. Pia kama simu umeroot simu yako basi njia hii ni rahisi zaidi.

WIFI WPS WPA TESTER
Price: Free

Baada ya kudownload App hii washa app hii kisha bofya kitufe cha duara upande wa kushoto juu kisha utaona inatafuta WiFi zote zilizopo karibu na wewe, kumbuka kuwasha router yako au kifaa chako cha WiFi ambacho umesahau password.

Baada ya kutafuta na kuona jina la WiFi yako, angalia kwa pembeni kwenye jina la WiFi yako kwenye app hiyo kama jina la WiFi yako lina kufuli la rangi ya kijani kwa pembeni basi unaweza kupata password ya WiFi hiyo.

Jinsi ya Kujua Password ya WiFi Yoyote (Kwa Kutumia Simu)

Lakini pia kama mbele ya jina la WiFi yako kuna kufuli la rangi nyekundu basi pengine ni vyema kujaribu njia ya pili kwenye makala hii. Kama kufuli mbele ya jina la WiFi yako ni rangi ya kijani basi endelea kwa kubofya hapo kisha chagua njia moja kati ya zilizo owanishwa, kumbuka kupata jina la Wifi yako inaweza kuchukua muda kutokana na ugumu wa password yako. Pia kama simu yako iko rooted basi kazi hii inachukua muda mfupi zaidi.

Kwa kutumia App ya ES File Explorer (Simu zilizoko Rooted)

Kwa wale ambao wame root simu zao basi unaweza kufuata njia hii ambayo mimi ndio iliyo nisaidia zaidi kwa kuwa nilikuwa na simu ambayo iko rooted. Njia hii ni rahisi lakini haitofanya kazi kwenye simu ambazo haziko rooted. Kama unataka kujifunza kuroot simu unaweza kusoma makala jinsi ya kuroot simu bila kutumia kompyua na pia jinsi ya kuroot simu yoyote ya tecno. Kumbuka kuwa makini wakati unaroot simu yakokwani unaweza kuharibu simu yako.

Kwa kuanza kama tayari umesha root simu yako unatakiwa kupakua app ya ES File Explorer kupitia link hiyo hapo chini. Baada ya kudownload endelea kufuata hatua hapo chini.

Baada ya kudownload App ya ES File Explorer fungua App hiyo kisha bofya Menu iliyoko upande wa kushoto kisha chagua Root Explorer.

Baada ya kuwasha sehemu hiyo, utaweza kuangalia file za ndani kabisa za simu yako hivyo kuwa makini usije kufuta kitu muhimu kwenye simu yako. Sasa peruzi kwenye file lililo andikwa “Data” kufungua file hilo kisha endelea kwenye hatua inayofuata.

Baada ya kufungua folder la Data ndani yeke utakutana na folder lingine linaloitwa “Misc“, fungua folder hilo kisha endelea kwenye hatua inayofuata.

Ndani ya folder la Misc unatakiwa kutafuta Folder lililo andikwa WiFi na ndani ya hilo folder kuna file lililo andikwa ‘wpa_supplicant.conf’ fungua file hilo ambalo utakuta lipo kwenye mfumo wa XML na kisha fuata hatua zinazofuata.

Sasa baada ya kufungua file hilo fafuta maneno SSID na pia tafuta PSK,SSID ni jina la WiFi yenyewe na PSK hiyo ndio password ya WiFi yenyewe. Copy file password hizo kisha weka kwenye WiFi yako na utaona tayari umeunganishwa na WiFi. Kumbuka wakati unafanya yote haya WiFi ya kifaa husika inatakiwa kuwa imewashwa.

Pia kumbuka ili kuweza kufanya hatua hizi unahitaji App hii ya pro hivyo app hiyo unaweza kuipata kwa kutumia link hapo chini.

Download ES File Explorer Pro

Na kwa kupitia njia hizi natumaini unaweza kupata password ya WiFi yako. Kumbuka tafadhali usitumie njia hii vibaya kwani nauhakika utapata tabu sanaaa. Kama utakuwa umekwama kwa namna yoyote tuulize kupitia kwenye maoni hapo chini au kupitia Tanzania Tech Forums.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use