Application 10 za Muhimu Kuwa Nazo Kwenye Simu Yako

Hizi hapa ni baadhi tu ya app ambazo ni vizuri kuwa nazo kwenye simu yako
App za muhimu kuwa nazo App za muhimu kuwa nazo

Wote tunajua watu wengi sana siku hizi wana simu janja a.k.a Smartphone, Lakini utakutana na watu wengi sana wakilalamika kuhusu simu zao kutokuwa nzuri na hii inasababishwa na watu hao kushindwa kujua programu gani za muhimu kutumia kwenye simu hizo ili kuweza kufurahia simu zao.

Najua wote tunakubaliana kwamba Smartphone haziwezi kuwa Smart bila kuwa na programu au Apps mbalimbali ndani yake. Sasa sababu hii na nyingine nyingi ndio zimepelekea leo tukutane hapa tujuzane Apps 10 za muhimu kuwa nazo kwenye simu janja yako. Kwa uzoefu nilionao na uhakika app hizi zitakusaidia kwa asilimia 100 hivyo chukua muda wako kusoma makala hii kwani na uhakika itakusaidia kwa namna moja ama nyingine. Basi kabla ujachoka kwa maneno mengi hebu twende kwenye list hii.

1. Nala

Pesa Money Manager
Price: To be announced

Kwanza labda tuanze na maswala ya pesa, Najua ni asilimia kubwa ya watu wanatumia huduma za kifedha kutoka kwenye simu zao, Sasa najua mitandao ya simu inakupa huduma nzuri tu pamoja na apps mbalimbali kwajili ya kurahisisha kufanya miamala.

Advertisement

Lakini app ya Nala ni nzuri zaidi kwani app hii inakupa uwezo wa kufanya miamala ya simu kutoka kwenye mitandao mbalimbali ya simu kwenye app moja, Utaweza kununua salio, kulipa bili mbalimbali na mengine mengi, uzuri wa app hii haubaki kwenye huduma hizo pekee bali unaweza kutumia app hii bila hata kuwa na Internet.

2. All tools na Smart Tools

All tools
Price: Free

Kama wewe ni binadamu na uko sawa kiakili nadhani ni lazima utahitaji app hizi. App hizi zinakupa vitu mbalimbali kwenye app moja yaani kwa mfano unaweza kupata tochi kama simu yako haina, barcode scanner, kipima size ya viatu, kuweka flash kwenye kamera ya mbele unapo piga picha usiku, Converter, Metal Detector na mengine mengi.

Kifupi ni kwamba unaweza kuona uhitaji app hizi lakini ukweli ni kwamba unahitaji app hizi kuliko hata unavyodhani kwani itatokea siku unataka kuwasha tochi kwenye simu yako isiyo na tochi na utakumbuka app hizi.

3. Tala na Branch

Tala Tanzania
Price: To be announced

Tukirudi tena kwenye swala la pesa, Najua kuwa kwa sasa huna haja ya mkopo, lakini labda ni kwambie tu ni muhimu sana kujiandaa na tatizo kabla halija tokea. Tala na Branch zinaweza kukusaidia sana kutatua matatizo yako madogo madogo na hii ni rahisi zaidi kama utakuwa unazo app hizi zote mbili.

Siku za karibuni mimi binafsi nime download app hizi kama sehemu ya majaribio. Baada ya kumaliza kujisajili na Tala nilifanikiwa kupata uwezo wa kukopa Tsh 20,000. Baadae nilipakua app ya Branch na baada ya kumaliza usajili nilifanikiwa kupata Tsh 10,000.

Sasa kwa kuwa sikua na shida ya mkopo kwa wakati huo nilichukua mkopo wa tala Tsh 10,000 na nikachukua na branch na baada ya siku moja nilirudisha mkopo wa Tala kwa kutumia pesa za Branch sasa naruhusiwa kukopa 50,000 Tala. Hii nimegeuza kama vikoba yani nakopa huku narudisha kule riba inatoka kwenye mikopo hii hii kwani sichukui kiwango kikubwa kuliko nachopewa na moja ya app hizi najua iko siku nitahitaji pesa hizi na nitakuwa na uwezo wa kukopa kiwango kikubwa.

4. Gazeti

Najua wengi wetu tunapenda kusoma habari, pia najua kuwa vyanzo vya habari hapa Tanzania ni vingi sana, sasa kwa sababu najua huwezi kudownload kila app ya habari na kuwa nayo kwenye simu yako basi wewe unakuwa unashindwa kupata habari zote kutokana na kuwa na chanzo kimoja cha habari. App ya Gazeti itakupa uwezo wa kusoma habari kutoka kwenye tovuti mbalimbali hapa Tanzania kupitia app moja. App hii pia inakupa uwezo wa kuangalia TV, kusikiliza Radio pamoja kuangalia video za matukio mbalimbali moja kwa moja kupitia simu yako.

5. Gbox

Hebu sasa tuamie kwenye upande wa mitandao ya kijamii, Tukianza na Instagram app ya Gbox ni moja kati ya app muhimu sana kuwa nayo. App hii inakupa uwezo wa kuongeza vitu muhimu kwenye picha zako lakini kitu cha muhimu kabisa ni njia ya kuweza kuona picha ya DP ya mtu kwa ukaribu na ikiwa kwenye Size kubwa. Najua unaweza kuanza kusema hii sio app ya muhimu lakini na uhakika wengi wetu tunatamani sana kuangalia DP ya mtu tena hasa kama mtu au akaunti fulani imewekwa Private.

6. Uber na Taxify

Uber - Request a ride
Bolt: Request a Ride

Kama wewe ni mmoja ya watu ambao hawana usafiri binafsi basi nakushauri download app za Uber na Taxify. App hizi ni muhimu sana hasa kwa watu wanaofanya safari za mara kwa mara, Najua unajua jinsi tulivyo hapa kwetu mtu anakuangalia jinsi ulivyo ndipo akwambie bei ya kusafiri na wakati mwingine unakuta uko na watu kiasi kwa huwezi kuanza kupatania bei hapo ndipo app hizi zinapokuja. Unaweza kutumia usafiri wa bajaj ndani ya app hizi na vilevile kupitia Taxify unaweza kupata hadi usafiri wa pikipiki.

Na hizo ndio app muhimu kuwa nazo kwenye simu yako kwa sasa, App hizi guys najua zinaweza kusaidia kwa namna moja ama nyingine, lakini pia kama unahisi kuna app ambayo inaweza kutoa imsaada mkubwa kwa watu na tumaisahau kwenye list hii basi tunaomba utukumbushe kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kama unataka kujua app nyingine nzuri za kuwa nazo kwa sasa unaweza kusoma hapa makala yetu iliyopita.

5 comments
  1. Yaani Kiongoz leo umenifanya nikachukia kwani Huduma zote za App ulizo leta Leo naona mapichapicha labda kidogo Nala cjatumia ila zingine kwangu zero hizo 10 za leo

    1. Sawa ila upende au usipende iko siku utahitaji moja ya app hizi ukiacha NALA. Pia wakati mwingine huwezi kujua unahitaji kitu mpaka uanze kukitumia.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use