in

Dili : Simu za Bei Nafuu Kuanzia Tsh 250,000 Kushuka Chini

Zifahamu hapa simu za bei nafuu ambazo unaweza kununua ukiwa na Tsh 250,000

Dili : Simu za Bei Nafuu Kuanzia Tsh 250,000 Kushuka Chini

Nadhani ni wazi kuwa siku hizi simu janja au smartphone zimeshuka bei sana, hii inachangiwa na ongezeko la simu mpya zinazo ingia sokoni kila siku kitu ambacho kinafanya simu za zamani kidogo kushuka bei na kuuzwa bei nafuu.

Kuliona hilo leo hapa Tanzania Tech tumewaletea list ya simu za bei nafuu ambazo zinauzwa chini ya shilingi za kitanzania Tsh 250,000. Kumbuka simu hizi unaweza kuzipata kupitia mtandao wa jumia hivyo ni muhimu kuwahi dili hili kabla ya muda kuisha yaani kabla simu hizo hazija nunuliwa.

Install Android App
Price: Free
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot

Kama unataka kununua moja ya simu kwenye list hii, bofya link chini ya maelezo ya simu na utapelekwa moja kwa moja kwenye mtandao wa Jumia tayari kununua simu husika. Basi bila kupoteza muda twende tuangalie simu hizi.

1. Galaxy J1 Mini Prime

Galaxy J1 Mini Prime ni simu ndogo lakini ni moja kati ya simu ambazo zinauwezo mkubwa wa kudumu na chaji na pia ni moja kati ya simu ngumu sana. Kama wewe ni mtu unaejali sana mawasiliano basi Galaxy J1 Mini Prime ni simu nzuri sana kwako.

Sifa na Bei ya Galaxy J1 Mini Prime

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 4.0
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 5.1
 • Processor – Quad-core 1.5 GHz au Quad-core 1.2 GHz, Spreadtrum SC9830 Chipset
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Kamera ya Mbele – VGA
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 5 yenye Flash ya LED
 • Ukubwa wa Ndani – GB 8
 • Mengineyo – Inayo Radio FM
 • Uinzi – Inatumia Pattern Haina Fingerprint
 • Bei – Tsh 200,000 – 250,000

NUNUA KWA TSH 199,000

2. Tecno Spark 2

Tecno Spark 2 ni moja kati ya simu nzuri sana na ni moja kati ya simu za hivi karibuni kutoka kampuni ya Tecno. Mbali ya kuwa ni nzuri sana kwa umbo, pia simu hii inakuja na uwezo wa kupakia programu za muhimu kama vile Instagram na mitandao mingine ya kijamii, simu hii ni nzuri sana kwa wapenzi wa picha na mitandao ya kijamii.

Sifa na Bei ya Tecno Spark 2

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.0
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo) Go Edition
 • Processor – Quad-core 1.3 GHz MediaTek Mt6580 Chipset
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Kamera ya Mbele – 8
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye Flash ya LED
 • Ukubwa wa Ndani – GB 16
 • Mengineyo – Haina Radio FM
 • Uinzi – Inayo Fingerprint kwa nyuma na Face Unlock
 • Bei – Tsh 300,000 – 350,000

NUNUA KWA TSH 245,000

3. Tecno Pouvoir 1

Tecno Pouvoir 1 ni moja kati ya simu maarufu sana kwa kudumu na chaji, mbali na hayo simu hii ni nzuri sana kwa umbo na inakuja na kioo kikubwa. Kama wewe ni mpenzi wa simu yenye kudumu na chaji hii ni kwaajili yako.

Sifa na Bei ya Tecno Pouvoir 1

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.0
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
 • Processor – Quad-core 1.3 GHz MediaTek MT6580 Chipset
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Kamera ya Mbele – 5
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 8 yenye Flash ya LED
 • Ukubwa wa Ndani – GB 16
 • Mengineyo – Haina Radio FM
 • Uinzi – Inayo Fingerprint kwa nyuma na Face Unlock
 • Bei – Tsh 300,000 – 350,000

NUNUA HAPA KWA TSH 149,000

4. Infinix Smart 2

Infinix Smart 2 ni moja ya simu nzuri sana kwa umbo na pia ni moja ya simu yenye uwezo mzuri sana wa kupiga picha. Kama wewe ni mmoja ya watu wanaopenda simu zenye kupiga picha vizuri basi simu hii ni kwaajili yako.

Sifa na Bei ya Infinix Smart 2

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
 • Processor – Quad-core 1.5 GHz Mediatek MT6739 chipset
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Kamera ya Mbele – 5
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye Flash ya LED
 • Ukubwa wa Ndani – GB 16
 • Mengineyo – Inayo Radio FM
 • Uinzi – Haina Fingerprint
 • Bei – Tsh 300,000 – 350,000

NUNUA KWA TSH 230,000

5. Tecno Pop 1 Pro

Kama ilivyo simu ya Spark 2, Tecno Pop 1 Pro nayo ni simu mpya kabisa kutoka kampuni ya Tecno. Simu hii inakuja na sifa za kawaida lakini ni moja kati ya simu nzuri yenye kuonekana vizuri sana mkononi. Kama wewe ni mmoja wa watu wanaopenda simu nzuri kwa bei nafuu basi simu hii ni kwaajili yako.

Sifa na Bei ya Tecno Pop 1 Pro

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 (Nougat)
 • Processor – Quad-core 1.3 GHz Mediatek Chipset
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Kamera ya Mbele – 5
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye Flash ya LED
 • Ukubwa wa Ndani – GB 16
 • Mengineyo – Haina Radio FM
 • Uinzi – Haina Fingerprint
 • Bei – Tsh 300,000 – 330,000

NUNUA KWA TSH 200,000

6. Tecno Spark K7

Tecno Spark K7 ni simu nyingine ya Tecno ya bei nafuu simu hii ni ya siku nyingi kidogo lakini ni moja ya simu ambazo bado ziko kwenye chati. Simu hii ni moja kati ya simu ambayo inakuja na kamera nzuri yenye kupiga picha vizuri.

Sifa na Bei ya Tecno Spark K7

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 (Nougat)
 • Processor – Quad-core 1.3 GHz Mediatek Chipset
 • Ukubwa wa RAM – GB 1 au GB 2
 • Kamera ya Mbele – 5
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye Flash ya LED
 • Ukubwa wa Ndani – GB 16
 • Mengineyo – Inayo Radio FM
 • Uinzi – Inayo Fingerprint kwa Nyuma
 • Bei – Tsh 250,000 – 350,000

NUNUA HAPA KWA TSH 250,000

7. Tecno F2

Tecno F2 ni simu nyingine pia ya bei rahisi kutoka kampuni ya Tecno, simu hii ni moja kati ya simu mpya kidogo kutoka kampuni ya Tecno, pia ni simu ambayo inaonekana kutumiwa na watu wengi sana pengine ni kwa sababu ya bei yake nafuu. Simu hii ni maalum kwaajili ya watu wanaolenga kuwasiliana zaidi.

Sifa na Bei ya Tecno F2

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 (Nougat)
 • Processor – Quad-core 1.3 GHz Mediatek Chipset
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Kamera ya Mbele – 2
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 5 yenye Flash ya LED
 • Ukubwa wa Ndani – GB 8
 • Mengineyo – Haina Radio FM
 • Uinzi – Haina Fingerprint
 • Bei – Tsh 200,000 – 300,000

NUNUA KWA TSH 180,000

8. Tecno Pop 1

Tecno Pop 1 ni simu ambayo ni ndogo ya simu ya Tecno Pop 1 Pro ambayo na inapatikana kwenye kist hii, simu hii haina tofauti sana na Pop 1 Pro bali simu hii yenyewe inakuja ikiwa na inauzwa kwa bei nafuu zaidi.

Sifa na Bei ya Tecno Pop 1

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 (Nougat)
 • Processor – Quad-core 1.3 GHz Mediatek Chipset
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Kamera ya Mbele – 5
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 5 yenye Flash ya LED
 • Ukubwa wa Ndani – GB 8
 • Mengineyo – Inayo Radio FM
 • Uinzi – Haina Fingerprint
 • Bei – Tsh 200,000 – 250,000

NUNUA HAPA KWA TSH 189,000

9. Tecno R6

Tecno R6 ni moja ya simu ya siku nyingi kidogo lakini pia ni simu ambayo hadi sasa bado inatumiwa na watu wengi. Simu hii inajulikana sana kwa kuwa simu ngumu sana kutoka kampuni ya tecno. Kama unataka simu inayodumu kwa muda mrefu badi Tecno R6 ni simu kwaajili yako.

Sifa na Bei ya Tecno R6

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.0
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 6.0
 • Processor – Octa core, 1.1 GHz Mediatek Chipset
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Kamera ya Mbele – 2
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 5 yenye Flash ya LED
 • Ukubwa wa Ndani – GB 8
 • Mengineyo – Inayo Radio FM
 • Ulinzi – Haina Fingerprint
 • Bei – Tsh 200,000 – 250,000

NUNUA KWA TSH 220,000

Na hizo ndio simu za bei nafuu chini ya Tsh 250,000 kama unataka kujua zaidi kuhusu simu nyingine za bei nafuu kuanzia Tsh 300,000 kushuka chini unaweza kusoma makala yetu ya simu za bei nafuu hapa. Kwa habari zaidi za teknolojia na dili mbalimbali za simu hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Google Kuzindua Simu Mpya za Pixel 8 Mwezi Oktoba (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments

 1. nahitaji kuanza biashara ya simu lakin niwe natoa nje na kuingiza nchini na natumai sana kuchukua china je itaniharimu kiasi gani kwa simu 50 za tecno tu makabilla tofauti please naomba msaana m by sanana