in

Zifahamu Hizi Hapa Bei na Sifa za Tecno Spark 2 (2018)

Hizi hapa ndio sifa kamili za simu mpya ya Tecno Spark 2

Sifa na Bei ya Tecno Spark 2
Muonekano wa Mbele wa Tecno Spark 2

Baada ya kusubiria kwa muda mrefu hatimae kampuni ya Tecno imezindua simu mpya ya Tecno Spark 2, simu hii kama tulivyo ona kwenye tetesi inakuja na sifa nzuri kwa matumizi ya kila siku pamoja na muonekano huku ikiwa na kioo kikubwa cha Full Display.

Hapa tutaenda kuangalia sifa za Tecno Spark 2, pamoja na kujua makadirio ya bei ya simu hii kwa hapa Tanzania. Simu hii inaendeshwa na processor ya MediaTek MT6580WP chip yenye Quad-Core processor na mfumo wa 64-bit CPU. Vilevile Tecno Spark 2 inakuja na processor yenye uwezo wa Cores nne 4 ambazo zina wezesha speed ya 1.4GHz. Kuwezesha game kufaya kazi kwa urahisi Tecno Spark 2 inakuja na GPU ya ARM Mali-400 MP2 graphics card yenye speed ya 416MHz. Tecno Spark 2 inatumia mfumo wa Android Go Oreo, mfumo ambao unafanya simu hii kuwa na RAM ya GB 1. Sifa nyingine za Tecno Spark 2 ni kama zifuatazo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Sifa za Tecno Spark 2

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.00 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 720 x 1440 pixels, 18:9 ratio (~274 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android GO 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – quad-core 1.3 GHz ARM Cortex-A7 MediaTek Mt6580 chipset
  • Uwezo wa GPU – Mali-400MP2
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 1
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 MP, f/2.4 dual-LED flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 autofocus, quad-LED flash
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3500 mAh battery
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Bluetooth v4.2, A2DP, LE
    pamoja na GPS ya A-GPS, microUSB 2.0
  • Rangi – Inakuja kwa rangi za Champagne Gold, Choral Blue, Metal Silver and Phantom Black
  • Mengineyo – Inayo Line Mbili za Dual SIM
  • Ulinzi – Fingerprint (iko nyuma), Face Unlock (kufungua simu kwa uso)
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G

Simu ya Tecno Spark 2 inakuja na kava la plastiki ndani ya box ambalo linakusaidia kuweza kulinda simu yako isiharibiwe na mikwaruzo, mbali na hayo simu hii inakuja na headphone, chaji na kadi ya warrant pamoja na kadi ya Boom Play. Tecno Spark 2 ni simu ya bei nafuu kwa ajili ya wapenzi wa simu za tecno.

Bei ya Tecno Spark 2 

Kwa upande wa bei ya Tecno Spark 2, simu hii inakuja kwa makadirio ya bei ya kawaida ya Tsh 300,000 hadi Tsh 350,000. Kumbuka bei inaweza kubadilika, Tecno Spark 2 inategemewa kuanza kupatikana hivi karibuni kupitia maduka ya Tecno pamoja na kwenye soko la mtandaoni la Jumia.

Zifahamu Hizi Hapa Bei na Sifa za Tecno Spark 2 (2018)
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

14 Comments