Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy A9s na Galaxy A6s

Zifahamu hapa hizi ndio sifa kamili za Samsung Galaxy A6s
Sifa na bei ya Galaxy A6s Sifa na bei ya Galaxy A6s

Kampuni ya Samsung bado inaendelea kuzindua simu zake mpya na hapo jana kampuni hiyo ilizindua simu mpya ya Galaxy A9s ambayo hii ni sawa na Galaxy A9 ambayo ilizinduliwa siku za nyuma, pamoja na Galaxy A6s ambayo hii ni simu ya kwanza ambayo haija tengenezwa na kampuni ya Samsung.

Tukianza na Galaxy A9s hii ni simu ambayo haina tofauti hata kidogo na simu ile yenye kamera nne kwa nyuma iliyo zinduliwa hivi karibuni, simu hii bado inakuja na sifa zile zile za kawaida za Galaxy A9 na hakuna kilicho badilika zaidi ya jina la simu hiyo tu ambapo nchini China inaitwa Galaxy A9 na sehemu nyingine duniani inaitwa Galaxy A9s.

Kwa upande wa Galaxy A6s yenyewe hii ni simu mpya kutoka Samsung, simu hii inakuja ikiwa inaripotiwa kuwa hii ndio simu ya kwanza ambayo inatengenezwa nje ya kampuni ya Samsung. Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali simu hii imetengenezwa na kampuni inayoitwa Wintech ambayo hii ndio hutengeneza simu za Xiaomi huko nchini China, kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya The Korea Herald hivi karibuni Samsung inatarajia kuacha kutengeneza simu kwaajili ya nchini China na kazi hiyo itachukuliwa na kampuni ambazo samsung itaingia nazo mkataba kwaajili ya kuunda simu kwaajili ya soko la nchini China.

Advertisement

Tukiachana na hayo, Twende tukaangalie yaliyomo kwenye simu hii mpya ya Galaxy A6s, Kwa kuanza Simu hii inakuja na kioo cha inch 6 chenye resolution ya 1080 x 2160 pixels ambacho pia kime tengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED Display. Galaxy A6s inaendeshwa na processor ya Snapdragon 660 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ndani wa kuchagua kati ya GB 64 pamoja na GB 128.

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili ambapo kamera kuu inakuja na Megapixel 12 na kamera nyingine inakuja na Megapixel 12 ambayo hii ni depth sensor. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera ya Selfie yenye uwezo wa Megapixel 12. Mbali na kamera simu hii inaendeshwa na battery ya Li-Ion yenye uwezo wa 3,300mAh battery ambayo bado haijajulikana kama inakuja na teknolojia ya Fast Charging au lah. Sifa nyingine za Galaxy A6s ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy A6s

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.0 chenye teknolojia ya Super AMOLED display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2160 pixels, 18:9 ratio (~402 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo).
 • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.2 GHz Cortex-A53.
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM660 Snapdragon 660 Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 506.
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja itakuwa na GB 64 na nyingine itakuwa na uwezo wa GB 128 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
 • Ukubwa wa RAM – GB 6.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 12 .
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko Mbili moja ikiwa na Megapixel 12 PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 12 PDAF zote zikiwa na phase detection autofocus na LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3300 mAh battery.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, Tyep C USB.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Black, White, Blue na Pink.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Micro-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint. (Kwa Nyuma).

Bei ya Samsung Galaxy A6s

Kwa upande wa bei simu hii inategemewa kupatikana kwa nchini China, na wote tunajua kinachopatikana china basi lazima Tanzania kitafika, hivyo unaweza kuipata simu hii kwa kuanzia Tsh 595,000 bila kodi ambayo hii ni sawa na Yuan ya China CNY 1,300. Toleo la ukubwa wa ndani wa GB 128 bado haijajulikana itauzwa Tsh ngapi. Endelea kutembelea Tanzania Tech kujua zaidi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use