in

Haya Hapa Maboresho Mapya Kwenye App za Instagram

Sasa unaweza kutuma picha zinazopotea kupitia instagram

Maboresho mapya Instagram

Mtandao wa instagram bado unaendela kufanyiwa maboresho mbalimbali kupitia app zake za Android na iOS. Moja ya maboresho ambayo Tanzania Tech tumegundua hivi karibuni ni pamoja na sehemu mpya ya Emoji pamoja na picha zinazopotea baada ya kuziangalia kwenye DM (Direct Message).

Tukianza na sehemu hiyo mpya ya Emoji, Instagram inafanya majaribio ya kuweka mtari mpya kwenye sehemu ya maoni au Comment ili iwe rahisi kwa watumiaji kuweza kutumia emoji kwenye sehemu ya maoni.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Sehemu ya hii kwa sasa ipo kwenye akaunti chache za Instagram kama sehemu ya majaribio, hivyo unaweza kuona sehemu hii au unaweza usione sehemu hiyo, kama unataka kuangalia kama sehemu hii iko kwenye akaunti yako ya instagram, fanya kama unataka ku-comment kwenye picha ya mtu yoyote utaona mstari maalum kama kwenye picha ya kwa au ya pili hapo juu.

Mabadiliko mengine ambayo tumeweza kuyaona kwa haraka haraka, ni sehemu ya kutuma picha mbayo inaweza kupotea mara baada ya uliye mtumia kuangalia picha hiyo. Sehemu hiyo inapatikana kwenye sehemu ya DM ambapo utaweza kutumia mtu picha ambayo inaweza kupotea baada ya yeye kuangalia picha hiyo.

Kupitia sehemu hiyo utaweza kuchagua picha unayomtumia mtu imfikie kwa aina tatu imfikie kwa njia ya kupotea baada ya kumfikia uliyemtumia, au kwa kumruhusu mtu aweze kujibu maoni yake baada ya kumtumia picha au pia kuacha picha ibaki kwenye sehemu ya uliyemtumia mpaka hapo atakapo jibu.

Hata hivyo mara baada ya uliyemtumia kupata picha hiyo ambayo inapotea, kutatokea mkanda wenye kuonyesha kama mfano wa cheche kwa juu na baada ya cheche hizo kuisha basi picha hiyo itapotea na hutoweza kuiona tena.

Sehemu zote hizo kwa sasa ziko kwenye majaribio kupitia kwenye programu ya Android ya Instagram hivyo unaweza kuona sehemu hizo au unaweza usione sehemu hizi. Vilevile bado hakuna taarifa kuhusu sehemu hizi kuja kwenye App za iOS pia bado hakuna taarifa lini watumiaji wote wataweza kupa sehemu hizi mpya.

Amani Joseph

Haya Hapa Maboresho Mapya Kwenye App za Instagram

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Apps Nzuri Kwaajili ya Kupakua Video za Aina Yoyote

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.