Instagram Yaleta Sehemu ya Kuonyesha Kama Upo Hewani

Sasa utaweza kujua kama mtu yupo hewani kwenye mtandao wa Instagram
instagram online instagram online

Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Instagram najua utakuwa umeona sehemu mpya kwenye mtandao wa Instagram, sehemu hii itaweza kuonyesha kama mtu yupo online kwenye mtandao huo wa instagram.

Sehemu hiyo ambayo sasa inapatikana kwenye mtandao huo, itaonyesha kidoti cha kijani pembeni ya jina la mtu kupitia sehemu ya DM ambapo kidoti hicho kitakuwa na maana mtu yuko hewani (Online) kwa muda huo kwenye mtandao wa Instagram. Kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, kidoti hicho cha kijani kitakuwa kinaonekana kwenye baadhi ya sehemu mbalimbali kama vile sehemu ya DM pamoja na wakati wa kushare picha na mfuasi (Follower) wako au mtu unae mfuata (Follow).

Instagram imekuwa ikibadilisha matumizi ya sehemu ya DM mara kwa mara, kwani siku za karibuni Instagram ilitambulisha App ya Direct kwaajili ya kuchati kupitia mtandao huo ikifuatiwa na sehemu ya kujua mtu alikuwa hewani kwa muda gani uliopita. Pengine hizi ni hatua za kubadilisha sehemu hiyo ya DM kuwa sehemu ya kuchati kama vile app za WhatsApp pamoja na Facebook Messenger.

Advertisement

Kwa sasa sehemu hii ya kidoti cha kijani inapatikana tayari kwenye App za mifumo yote ya Android pamoja na iOS. Kwa mujibu wa ripoti sehemu hii itatokea kwa watu uliowafuata (Follow) au walio kufuata (Followers) ikiwa pamoja na watu ambao tayari ulisha chati nao kupitia sehemu ya DM.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use