in

Apps# 8 Jaribu App Hizi Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android

Jaribu sasa App hizi nzuri kwenye simu yako ya Android

Apps# 8 Jaribu App Hizi Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android

Karibuni tena kwenye Awamu nyingine ya App nzuri za Android ambazo unaweza kujaribu kwenye simu yako. Kama wewe ni mgeni ni vyema ufahamu kuwa, kila wiki tunakuwa na nafasi ya kuangalia Apps mbalimbali za Android ambazo tunaimani zitaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kurahisha matumizi ya simu yako au kufanya uweze kufurahia matumizi ya simu yako ya Android kwa namna moja ama nyingine.

Hivyo basi, kama unapendelea kujaribu Apps mpya kwenye simu yako hasa ya Android, basi hakikisha unatembelea Tanzania Tech angalau mara moja kwa wiki ili uweze kujaribu App mpya na nzuri kwenye simu yako ya Android. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie Apps nzuri za wiki hii.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

1. Quick Dictionary

Application hii itakusaidia kuweza kupata Dictionary kwa haraka na utaweza kupata tafsiri ya maneno mbalimbali kwa haraka bila kupoteza muda. Download app hii kisha bofya sehemu ya Copy Service kuweza kuwasha app hii na uweze kupata tafsiri ya maneno ya kingereza kwa haraka.

2. Versus

Versus
Price: Free

Versus ni App nyingine nzuri ya Android inayokupa uwezo wa kulinganisha tofauti ya vitu mbalimbali ikiwa pamoja na Simu, Tv kompyuta na vitu vingine mbalimbali app hii ni rahisi kutumia na ni moja kati ya App nzuri sana za android kwaajili ya kukusaidia kununua vitu.

3. PixelKnot: Hidden Messages

Kama umekuwa ukitaka kuficha meseji zako mtu asiweze kuziona basi app hii ni muhimu kwako, App hii itakuwezesha kutuma meseji ikiwa imefichwa kwenye picha na mtu yeyote hatoweza kuiona mpaka awe na app hiyo pamoja na password maalum. Unaweza kushiriki picha hiyo kwenye mitandao ya kijamii na watu wengine wataona picha hiyo kama kawaida lakini kwa kutumia app hii utaweza kuona meseji iliyo jificha juu ya picha uliyotuma.

4. MomentCam Cartoons & Stickers

Kama umekuwa ukitamani kutengeneza katuni yenye kufanana na sura yako basi app hii ni nzuri kwako, App hii itakupa uwezo wa kutengeneza katuni zenye kufanana na sura yako kwa asilimia 99 na utaweza kushiriki picha hizo kwenye mitandao ya kijamii au kuhifadhi kwenye simu yako.

5. Neverthink

Kama umekua ukitafuta mambo mazuri ya kuangalia kwenye mitandao mbalimbali basi App hii ni nzuri sana kwako, App hii itakuruhusu kuweza kuangalia video mbalimbali za muhimu kwa kuchagua aina ya video unazopenda. Utaweza kuchagua kwa kubofya kitufe kimoja tu na utaweza kuangalia video moja kwa moja.

Na hizo ndio App nilizo kuandalia kwa siku ya leo unaweza kutembelea ukurasa huu ili kujua app nyingine nzuri za kuweza kujaribu kwenye simu yako ya Android.  Kumbuka leo ndio siku ya mwisho kuweza kujishindia Vocha ya Tsh 10,000 hakikisha unatembelea Ukurasa Huu kuweza kushiriki na kujipatia Vocha Yako.

App ya ChatGPT Inapatikana Kwa Watumiaji wa Android

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments