in

Simu Mpya za Tecno Ulizokua Huzijui Mwaka Huu (2019)

Hizi hapa simu mbili mpya za tecno ambazo huenda ulikua huzijui

Simu za Tecno
Picha ya Tecno Camon i

Simu za Tecno ni moja kati ya simu zenye wa tumiaji wengi sana kwa hapa Afrika, lakini pamoja na simu hizi kuwa na watumiaji wengi sio simu zote za tecno zinazotoka nchi zingine zinafanikiwa kufika Tanzania kwa wakati.

Sasa leo nimekuandalia simu mbili mpya za tecno ambazo zilizinduliwa mwaka huu 2019 lakini kwa sasa bado hazijafika Tanzania. Wote tunajua sio kila simu za tecno zina pozinduliwa watu wanajua, bali kuna simu zingine ukienda sokoni tu unakutana nazo bila kujua hata zilizinduliwa lini. Sasa kuhakikisha hupitwi tutakua tunakuletea simu zote za tecno pale zinapo zinduliwa hata kama bado hazijafika hapa Tanzania.

Install Android App
Price: Free
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa kuanza leo tumefanya jitihada ya kupata simu za tecno mbili ambazo mpaka sasa nadhani bado hazijafika Tanzania, ila na hakika siku za karibuni utashitukia tu simu hizi ziko kwenye maduka mbalimbali ya simu. Simu zenyewe ni Tecno Camon I pamoja na Tecno Camon I Air.

Tecno Camon i (2018)

Simu hii mpya ya Tecno Camon I imezinduliwa hivi karibuni January 29 mwaka huu 2018, simu hii inakuja na kioo cha kisasa kama ilivyo simu ya Tecno Camon CM iliyozinduliwa mwaka huu 2018. Vitu vingine vya msingi kwenye Simu hii ya tecno camon i, ni pamoja na uwezo mzuri sana wa battery pamoja na uwezo mkubwa wa ndani wa hadi GB 32.

Sifa kamili za Tecno Camon i (2018)

 • Uwezo wa Kioo – inch 5.65″ (14.35 cm) chenye resolution ya 720 x 1440 pixels.
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android v7.0 (Nougat) operating system.
 • Uwezo wa Processor – Quad core, 1.3 GHz, Cortex A53 processor.
 • Uwezo wa RAM – GB 3
 • Ukubwa wa Ndani – GB 32 unaweza kuongeza kwa memory ya hadi GB 128.
 • Uwezo wa Kamera – Simu Hii ina uwezo wa Kamera za Megapixel 13 kwa mbela na nyuma
 • Uwezo wa GPU – Mali-T720 MP2 GPU
 • Uwezo wa Battery – Battery ya Li-ion ambayo haitoki yenye 3050 mAh.
 • Mengine ya muhimu – Inakuja na Radio, Uwezo wa 4G, Bluetooth v4.0, WiFi 802.11, b/g/n, Pamoja na uwezo wa Laini mbili.
 • Bei –  Inauzwa kwa rupee za kihindi ₹ 8600 sawa na Tsh 300,000 kwa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo. (Bei inaweza kubadilika kwa Tanzania).

Tecno Camon i AIR

Siku chache baada ya tecno kuzindua simu ya Tecno Camon i kwenye tarehe 6 mwezi wa pili tecno ilizindua tena simu mpya ya tecno camon i Air simu hii ikiwa ni toleo la pili la Camon i. Sasa simu hii inafanana kila kitu na simu hiyo ya mwanzo lakini simu hii ya Camon i Air inakuja na ukubwa mdogo wa ndani, RAM ndogo pamoja na kamera ndogo ya mbele.

Sifa kamili za Tecno Camon i Air

 • Uwezo wa Kioo – inch 5.65″ (14.35 cm) chenye resolution ya 720 x 1440 pixels
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android v7.0 (Nougat) operating system.
 • Uwezo wa Processor – Quad core, 1.3 GHz, Cortex A53 processorr.
 • Uwezo wa RAM – GB 2
 • Ukubwa wa Ndani – GB 16 unaweza kuongeza kwa memory ya hadi GB 128.
 • Uwezo wa Kamera – Simu Hii ina uwezo wa Kamera ya Mbele Megapixel 8 na kamera ya nyuma Megapixel 13.
 • Uwezo wa GPU – Mali-T720 MP2 GPU
 • Uwezo wa Battery – Battery ya Li-ion ambayo haitoki yenye 3050 mAh.
 • Mengine ya muhimu – Inakuja na Radio, Uwezo wa 4G, Bluetooth v4.0, WiFi 802.11, b/g/n, Pamoja na uwezo wa Laini mbili.
 • Bei –  Inauzwa kwa rupee za kihindi ₹ 7999 sawa na Tsh 280,000 kwa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo. (Bei inaweza kubadilika kwa Tanzania).

Na hizo ndio simu za tecno ambazo huenda ulikua huzifahamu, simu hizi zitakuwa madukani kwa namna moja ama nyingine hivyo ni vyema umesoma makala hii. Kujua zaidi kuhusu simu za tecno pamoja na bei zake soma makala hii hapa. Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech.

Angalia Uzinduzi wa iPhone 15 Ndani ya Dakika 17

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments