in

Jinsi ya Kujua Simu Original ya Tecno Pamoja na Battery Yake

Njia rahisi ya kuhakikisha kama simu na battery ya Tecno ni Original

Jinsi ya Kujua Simu Original ya Tecno Pamoja na Battery Yake

Karibuni kwenye maujanja ya Tanzania Tech, leo tutaenda kuangalia njia ya kisasa ya kujua kama simu yako ya Tecno ni original ikiwa pamoja na jinsi ya kuangalia kama battery ya simu yako ya Tecno ni original, hii ni kwa wale ambao simu zao zinafunguka mifuniko ya sehemu ya battery.

Kama tunavyojua tecno ni moja kati ya simu zinazo tumika sana hasa hapa Afrika na Tanzania kwa ujumla, lakini kutokana na simu hizi kuwa na wateja wengi kuna wakati wafanya biashara wasiokuwa waaminifu hutumia njia zisizo za alali kuleta na kuuza simu za Tecno ambazo sio Original. Vilevile baadhi ya wafanya biashara hawa pia hutumia njia ambazo sio za uaminifu kubadilisha vifaa mbalimbali vya simu za Tecno na kuweka vifaa feki na hii kumu-umiza mteja kwa namna moja ama nyingine.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Sasa kuliona hili leo nimekuletea njia rahisi sana na ya uhakika ya kuangalia simu ya Tecno pamoja na battery yake kama ni Original, njia hii ni rahisi sana kutumia na unaweza kuifanya wakati wowote pale unapokua unataka kununua simu ya tecno au hata pale unapotaka kununua battery ya simu yako ya Tecno.

Kwa kuanza basi ni mahitaji ni lazima uwe na internet angalau hata MB 10, haijalishi unatumia kifaa gani iwe simu au kompyuta unaweza kufanya hatua hizi kwa urahisi kabisa, kisha kama unataka kuangalia kama simu yako ya Tecno ni Original basi fuata hatua hizi.

Hatua ya kwanza ingia kwenye ukurasa huu (bofya hapa) > http://gc.tecno-mobile.com kisha chukua simu yako ya Tecno kisha soma namba ya IMEI Code ( una weza kupata IMEI Code kwa kubofya *#06# kwenye simu yako ya Tecno) pamoja na namba nyingine ya VC code kisha ingiza namba hizi kwenye ukurasa wa Tecno ulio fungua awali kisha bofya Submit.

Baada ya hapo utaletewa maandishi ya kukwambia kama simu yako ni Original au ni feki, njia hii ni rahisi kutumia na ni ya haraka. Vilevile kama unataka kuangalia kama battery ya simu yako ya Tecno ni Original unaweza kutembelea ukurasa ule ule http://gc.tecno-mobile.com, kisha kwa chini utaona maneno Genuine Battery Check chukua battery yako ya simu ya Tecno kisha soma namba zilizo andikwa SN code kisha ziandike kwenye sehemu ya Genuine Battery Check, baada ya kumaliza bofya Submit baada ya hapo utaletewa maelezo ya kukwambia kama battery ya simu yako ya Tecno ni Original au feki.

Natumaini maujanja haya yameweza kukusaidia au yataweza kukusaidia kwenye siku za usoni, pia kama unataka simu origanl ya Tecno unaweza kuangalia list ya simu bora za Tecno kununua kwa mwaka huu 2018 na uhakika lazima utapata simu bora kwaajili yako. Basi mpaka siku nyingine tena endelea kutembelea Tanzania Tech ili kujifunza maujanja zaidi.

Amani Joseph

Jinsi ya Kujua Simu Original ya Tecno Pamoja na Battery Yake

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kufufua Spika ya Simu Yako Bila Kufungua

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

10 Comments