in

Sifa za Simu Mpya za Samsung Galaxy A8 na Galaxy A8 Plus (2018)

Sasa simu hizi zina muonekano kwama wa simu za Samsung Galaxy S8

Samsung Galaxy-A8-2018 na Samsung Galaxy A8 Plus

Hivi karibuni kampuni ya Samsung imezindua simu zake mpya za kwanza zenye muundo unao karibiana na simu za Samsung Galaxy S8. Simu hizi za Samsung Galaxy A8 na Samsung Galaxy A8 Plus zote za mwaka 2018 zinakuja na kioo cha infinity Displays pamoja na sifa nyingi za kipekee kabisa.

Install Android App
Price: Free
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot

Samsung Galaxy A8 2018 na Samsung Galaxy A8 Plus 2018 ni simu zilizo fanana lakini zimetofautiana kidogo kisifa na kwa ukubwa, kwa kuanza ngoja tuangalie sifa za Samsung Galaxy A8 (2018).

Sifa za Samsung Galaxy A8 (2018)

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.6 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive na Resolution ya 1080 x 2220 pixels na ratio ya 18.5:9
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android Nougat 7.1.1
 • Uwezo wa Processor – Inatumia Processor ya Exynos 7885 Octa yenye uwezo wa Octa-core 2×2.2 GHz pamoja na GPU ya Mali-G71.
 • Ukubwa wa Ndani – Inaukubwa wa ndani wa kuchagua kati ya GB 32 na GB 64
 • Uwezo wa RAM – Inatumia RAM ya GB 4
 • Kamera ya Mbele – Kamera ya mbele inauwezo wa Megapixel 16 huku ikiwa na uwezo wa f/1.7, phase detection autofocus na LED flash.
 • Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na uwezo wa Megapixel 16 na nyingine ikiwa na Megapixel 8 zote zikiwa na uwezo wa kuchukua video na picha za f/1.9 pamoja na 1080 pixel.
 • Uwezo wa WiFi – Ina wifi yenye uwezo wa 802.11 a/b/g/n/ac pamoja na teknolojia za dual-band, WiFi Direct na hotspot.
 • Uwezo wa Bluetooth – Inatumia bluetooth ya 5.0, A2DP, EDR, LE
 • Viunganishi Vingine – Inatumia teknolojia ya NFC, pia inayo Radio FM pamoja na USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector
 • Uwezo wa Sensor – Inatumia Sensor za Fingerprint (rear-mounted), accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer.
 • Uwezo wa Battery – Inatumia Battery ambayo haitoki ya Li-Ion yenye uwezo wa 3000 mAh
 • Bei – Euro 500 sawa na dollar za marekani $593.57 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,330,000 hii ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilishia fedha vya leo (bei inaweza kubadilia kwa Tanzania).

Sifa za Samsung Galaxy A8 Plus (2018)

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.0 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive na Resolution ya 1080 x 2220 pixels na ratio ya 18.5:9
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android Nougat 7.1.1
 • Uwezo wa Processor – Inatumia Processor ya Exynos 7885 Octa yenye uwezo wa Octa-core 2×2.2 GHz pamoja na GPU ya Mali-G71.
 • Ukubwa wa Ndani – Inaukubwa wa ndani wa kuchagua kati ya GB 32 na GB 64
 • Uwezo wa RAM – Inatumia RAM ya GB 4 kwa simu yenye ukuwa wa Ndani wa GB 32 na RAM GB 6 kwa simu yenye ukuwa wa ndani wa GB 64
 • Kamera ya Mbele – Kamera ya mbele inauwezo wa Megapixel 16 huku ikiwa na uwezo wa f/1.7, phase detection autofocus na LED flash.
 • Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na uwezo wa Megapixel 16 na nyingine ikiwa na Megapixel 8 zote zikiwa na uwezo wa kuchukua video na picha za f/1.9 pamoja na 1080 pixel.
 • Uwezo wa WiFi – Ina wifi yenye uwezo wa 802.11 a/b/g/n/ac pamoja na teknolojia za dual-band, WiFi Direct na hotspot.
 • Uwezo wa Bluetooth – Inatumia bluetooth ya 5.0, A2DP, EDR, LE
 • Viunganishi Vingine – Inatumia teknolojia ya NFC, pia inayo Radio FM pamoja na USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector
 • Uwezo wa Sensor – Inatumia Sensor za Fingerprint (rear-mounted), accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer.
 • Uwezo wa Battery – Inatumia Battery ambayo haitoki ya Li-Ion yenye uwezo wa 3500 mAh
 • Bei – Euro 600 sawa na dollar za marekani $712.28 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,600,000 hii ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilishia fedha vya leo (bei inaweza kubadilia kwa Tanzania).

Na hizo ndio sifa za simu mpya za Samsung Galaxy A8 (2018) na Samsung Galaxy A8 Plus (2018). Je unaonaje simu hizi tuambia maoni yako kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Simu Mpya za iPhone 15 Pro na 15 Pro Max (Mabadiko Muhimu)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

3 Comments

 1. Ninapata shida ku update galaxy A8
  plus .Niliinunua Dubai na nimegundua kuwa imesajiliwa UAE . Kila nikijaribu ku update sofware inaonyesha kuwa latest software update are installed. Kwa uelewa wangu mdogo naamini kuwa haiwezi kupokea updates kwa vile sio registered globally.
  Naomba msaada tafadhali.

  • Hapana kupokea update haitegemeani sana na nchi uliyopo bali aina ya simu uliyonayo, kama unayo simu ambayo inapokea update sasa kwenye nchi nyingine basi ni lazima hizo update zitakuja hata hapa Tanzania. Kizuri ni kuwa kuna wakati ukiwa na simu ya nchi fulani unaweza kupata update kwa kuchelewa au wakati mwingine kwa kuwahi.

   • Nashukuru kwa maelezo mazuri. Wasiwasi wangu kwa hii simu yangu ni kuwa baada ya kuichunguza nimegundua kuwa ile sehemu ya Hardware version kumeingizwa details za Dubai.
    Kama hivi.. United Arab Emirates
    TRA ID:0016333/08
    TA:00000000/00
    JE kwa details hizo hapo juu ,sio kweli kuwa itaweza kupata software updates pale tu nitakapoweka sim card ya mtandao wa Dubai ? ua