Zifahamu Hapa Sifa za Honor V10 Simu Mpya Kutoka Huawei

Sasa simu hii inakuja na Kioo cha Inch 5.99 na Ukubwa wa GB 128
Honor-V10 Honor-V10

Mapema siku ya jana kampuni ya Honor ambayo ni sehemu ya kampuni ya Huawei ilizindua simu yake mpya ya Honor V10 huko mjini Beijing nchini China. Simu hiyo ambayo imekuja na kioo kikubwa na processor yenye nguvu, inasemekana kuwa sifa zake ni kama vile mchanganyiko wa simu za Huawei Mate 10 pamoja na Huawei Mate 10 Pro.

Pamoja na simu hiyo kuwa bora bei yake pia inasemekana kuwa rahisi zaidi kuliko hata ile ya simu za Huawei Mate 10 pamoja na Huawei Mate 10 Pro, vilevile simu hii inakuja na mfumo mpya wa Android 8 Oreo pamoja na processor yenye nguvu ya Kirin 970 ikiwa imewezeshwa na mfumo wa AI au Artificial Intelligence. Kujua sifa zake kamili Honor V10 ina –

Advertisement

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.99 huku kikiwa kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD, yenye uwezo wa kuonyesha rangi milioni 16.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 Oreo ulio boreshwa kwa kuwekewa mfumo wa Huawei wa EMUI 8.0.
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.4 GHz Cortex-A73 & 4×1.8 GHz Cortex-A53) yenye GPU ya Mali-G72 MP12.
  • Ukubwa wa Ndani – Zinakuja aina mbili GB 128 na GB 64.
  • Uwezo wa RAM – Zinakuja aina mbili, simu yenye ukubwa wa ndani wa GB 128 inakuja na RAM ya GB 6 na Simu yenye Ukubwa wa Ndani wa GB 64 inakuja na RAM ya GB 4.
  • Kamera ya Mbele – Megapixel 13, yenye uwezo wa f/2.0
  • Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ina Megapixel 16 yenye uwezo wa f/1.8 na nyingine inayo Megapixel 20 zote zikiwa na uwezo wa kuchukua video za 2160p@30fps pamoja na uwezo wa phase detection autofocus,Geo-tagging, touch focus, face/smile detection, panorama pamoja na HDR.
  • Uwezo wa Bluetooth – 4.2, A2DP, aptX HD, LE
  • Uwezo wa Wireless – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n/ac, dual-band yenye WiFi Direct na hotspot
  • Uwezo wa GPS – A-GPS, GLONASS, BDS
  • Uwezo wa Battery – Inakuja na Battery ambayo haitoki ya Li-Po yenye uwezo wa 3750 mAh.
  • Uwezo wa Fast Charging – Inakuja na uwezo wa Fast battery charging 4.5V/5A yenye uwezo wa kujaza asilimia 58 kwa dakika 30.
  • Aina ya Charger inayotumia – 2.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tofauti nne yaani Beach Gold, Aurora Blue, Charm Red na Night Black
  • Bei – Inapatikana kuanzia dollar za marekani $498 au $500 ambayo ni sawa na shilingi za Tanzania Tsh 1,120,000 (kumbuka bei kwa mujibu wa viwango vya fedha hivyo inaweza kubadilika).

Na hizo ndio sifa za simu hiyo mpya ya Huawei Honor V10 iliyotoka rasmi hapo jana, simu hii itanza kuingia sokoni kuanzia mwezi December hivyo kwa Tanzania kuipata itakubidi usubiri mpaka mwezi February mwakani yaani 2018.

Nini maoni yako kuhusu simu hii, je ina sifa bora kuliko simu za Huawei Mate 10 na Huawei Mate 10 Pro..? tujulishe kwenye maoni hapo chini. Kwa habari zaidi usasahau kudownload App ya Tanzania Tech kama unatumia simu yenye mfumo wa Android.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use