in

Jinsi ya Kuondoa Lock ya Android Bila Kuflash au Kureset Simu

Kama simu yako inayo Pattern au Lock ya aina yoyote na umesahau soma hii

kuondoa Lock

Kutokana na ulimwengu wa teknolojia kuwa mpana kila siku sio ajabu unaposikia mtu akikwambia nimesahau password au pattern za simu yangu, hii ikiwa ni matokeo ya teknolojia kuwa kubwa sana kiasi kwamba kila kitu unakuta kinatumia password hivyo kutokana wingi wa vifaa ni rahisi sana kusahau pattern au password yako. Kuliona hilo leo Tanzania Tech tunakuleta njia ya kuondoa pattern au password yoyote ile kwenye Android bila kupoteza data zako kabisa!.

Kwa kuanza ni vyema kujua vitu vichache ambavyo vita kusaidia. Njia hii itakusaidia endapo kama utakuwa umewasha USB Debugging kwenye simu yako (hii ni muhimu sana) bila kufanya hivi njia hii haita fanya kazi hivyo ni vyema ujue kuwa simu yako imewashwa USB Debugging sehemu hii inawashwa kwa kufuata njia hizi (bofya hapa kuzijua). Vilevile unatakiwa kuwa na ADB Drivers za simu yako ili kupata driver hizo Bofya hapa kisha download ADB Driver Installer install kwenye kompyuta yako kisha endelea kwa kufuata hatua hizi.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Baada ya kuinstall driver zako moja kwa moja download programu ya Android SDK Tools kwaajili ya Windows Hapa na kwaajili ya Mac Hapa na kama unatumia Ubuntu au chrome OS bofya Hapa, fungua programu hiyo kisha chagua na install programu hiyo kama inavyonekana kwenye picha hapo chini.

Ukisha maliza kuinstall fungua mahali ulipo install programu hiyo kisha fungua Android SDK Tools Users > App Data > Local > Android > Android-SDK > Platform-Tools kisha shikilia control kwenye keyboard ya kompyuta yako kisha right click kwa kurumia mouse yako kisha bofya open command window here.

 

Baada ya hapo sehemu ya command itafunguka chomeka simu yako kisha subiri kidogo kisha bofya hap chini kwenye view raw au bofya hapa kisha copy code hizo na paste kwenye command ya kompyuta yako uliofungua awali kisha bofya Enter kisha subiri kidogo kisha restart simu yako.

Kama code hizo hazitofanya kazi kwenye simu yako basi tumua code hizi hapa chini kujaribu tena kufungua simu yako, kama awali copy na paste kwenye command uliofungua awali kisha bofya Enter.

Baada ya kurestat simu yako utaona pattern au lock ya simu yako imeondoka kabisa na hapo utakuwa umewezesha simu yako kuondoa lock screen au pattern ya aina yoyote kwenye simu yako ya Android. Kama kuna mahali umekwama usisite kutandikia kwenye maoni hapo chini nasi tutakujibu moja kwa moja.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.

Rahisisha Mambo Mbalimbali kwa Kutumia Tovuti Hizi

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

21 Comments

  1. Maoni*Naomba msaada wenu wataalamu wa simu,
    Simu yangu ina tatizo la kujiwasha data yenyewe ;nikizizima inajiwasha baada ya sekunde chache.Nimejaribu kui-restart bado tatizo liko palepale.Nifanyeje?

  2. Mimi naitwa Dativa Majaliwa natumia simu aina ya infinix nilisahau pattern ikafungiwa sasa nitafanyaje kuifungua bila kutumia computer maana niko bukoba vijijini hamna mtu mwenye computer huku mswada wenu please