in

Jinsi ya Kurudisha Picha Zilizofutika Kwenye Simu Yako ya Android

Jinsi ya Kurudisha Picha Zilizofutika Kwenye Simu Yako ya Android

Kuna wakati inatokea unafuta picha zako kwenye simu yako kwa bahati mbaya au hata kuna muda tu unataka kurudisha picha zako ulizowahi kuzifuta kutoka kwenye simu yako kama unataka kufanya hayo yote basi usijali kwani leo tutaenda kujifunza namna rahisi ya kurudisha picha zako hizo kwenye simu yako kwa namna rahisi kabisa.

Hata hivyo kama inavyojulikana watu wengi sana wanajua namna ya kurudisha picha zilizopotea kwenye kompyuta lakini watu wengi hawajui kufanya hivyo ikija katika swala zima la Smartphone au (Android Phones) au hata simu nyingine za mkononi, hivyo basi leo tutajifunza hatua kwa hatua namna ya kufanya hivyo bila kutumia muda mwingi.

Kwa kuanza basi ili kuweza kufanikisha hili unahitaji kuwa na bando atlist MB100 kwaajili ya kupakua programu kutoka kwenye PlayStore kingine unatakiwa kuhakikisha kuwa simu yako iko ROOTED (Bofya hapa kuangalia namna ya ku-root simu yako) ukisha fuata maelezo hayo na kuhakikisha simu yako iko rooted endelea kipengele cha pili ambapo ni kupakua Programu ya Android iitwayo (DiskDigger) bofya hapo chini kupakua programu hiyo ya android kwenye simu yako.

Jinsi ya Kugundua Mapema Tatizo Lolote la Simu Yako

Baada ya hapo install programu hiyo kisha ruhusu programu hiyo kupitia superuser  baada ya hapo chagua file lenye picha zilizo potea alafu chagua format kama ni jpg, png au hata mp4 kisha acha programu hiyo ifanye scaning baada ya hapo moja kwa moja utaweza kurestore picha zako na hata video.

Kama umeipenda hii usisite kulike page yetu ya Facebook pamoja na Twitter ili kupata habari mpya pindi zinapotoka, pia kwa kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo unaweza ku subscribe kwenye Youtube Channel yetu hapa Tanzania tech blog. Pia usisahau kubofya hako ka-LOVE hapo chini ili ku-show love..!!

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

32 Comments

  1. mimi nimefuta picha zangu lakini kila nkidownload hazikubali kwa nini naomba mnisaidie au nipigieni kwenye namba hii 0776333022 au 0719882437 niwafuate popote mulipo na ntalipa gharama zote kwenye wasap ukisevu namba hii utaniona au fb email yangu ni suleimanali1364@gmail.com nipo unguja mtu yoyote atakae uona ujumbe huu naomba anisaidie