YouTube Yafanya Majaribio ya YouTube Messenger

Youtube Messenger Youtube Messenger

Hivi karibuni youtube imeanza kufanya majaribio ya kuleta program ya chatting kwenye mtandao wake maarufu wa youtube, ikiwa siku mbili zimepita toka mtandao huo kutangaza hivyo ni watu wachache tu wanaoweza kuiona sehemu hiyo mpya.

Hata hivyo mabadiliko hayo ni kwa upande wa programu zake za Android pamoja na iOS tu, akiwa anaelezea jinsi inavyotumika kiongozi mmoja kutoka youtube alisema ” mtumiaji anaweza kutuma video kwa rafiki, ndugu na jamaa na pale mtumiaji wa upande wa pili anapo pokea video hiyo hapo wanaweza kuanza kuchati kwa kuandika ujumbe mfupi pia kila mmoja anaweza kumu-unganisha mtu amtakaye kwenye chat hiyo”.

Hata hivyo watu wengi duniani wanasema kuwa sehemu hiyo mpya itasaidia sana kufanya mtandao huo kupendwa na hata watu wengi zaidi dunia, hata hivyo hii ni sehemu moja wapo ya mpango wa kuboresha mtandao huo ambapo mwaka jana Youtube ilitangaza kuanza kuonyesha video online pamoja na offline.

Advertisement

Vilevile youtube kwa kupitia wasemaji wake haikutangaza kwamba sehemu hiyo mpya itaanza kutumiaka lini rasmi bali wasemaji hao walisema “bado programu hii iko kwenye majaribio na ni mapema sana kusema itatoka lini lakini tunapenda kuwaambia wapenzi wa mtandao wetu kuwa wakae tayari kwani kuna mambo mengi mazuru yanakuja”.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use