Mtandao wa Facebook na Instagram Wazuiwa Vietnam

Fcebook Imefungwa Fcebook Imefungwa

Mitandao maarufu ya facebook pamoja na instagram imezuiwa huko vietnam kwa sababu ya kile kinachosemekana ni uchochezi wa vurugu baina ya wananchi na kampuni ya cha chuma inayomilikiwa na Taiwan’s Formosa Plastics, sakata hilo lilichukua hatua mpya baada ya wananchi kuanza kuandamna wakitaka kiwanda hicho kifungwe kwa kusababisha uchafuzi wa mito ambayo wakazi hao wa vietnam hutumia kama chazo cha kujipatia kitoweo cha samaki.

Hata hivyo inasemekana kuwa maandamano hayo ya lisabishwa na mitandao hiyo ya kijamii kwani imekua ikitumika kama chanzo cha kukutanisha watu ili kufanya maandamano hayo, pia watu wamekua wakituma picha mbalimbali za watu walioshika mabango ya kushinikiza kufungwa kwa kiwanda hicho ambapo serikali ya vietnam imesema huo ni kama uchochezi kwani watu wamekuwa wakitoa maoni mbalimbali kwenye picha hizo na kusababisha vurugu kuendela kushamiri. Tayari zaidi ya watu 300 wamekamatwa katika mji wa Ho Chi Minh pamoja na Paris Square, watu wengi wameonekana kujeruhiwa wakati polisi wakikamata watu kutoka kwenye makundi mbalimbali ya watu waliokuwa wakileta vurugu hizo.

Serikali ya vietnam inakanusha kuwa kiwanda hicho akiusiki na vifo vya samaki kwenye mito na mabwawa hayo ambayo utumika na wananchi kama sehemu ya muhimu ya kujipatia kipato na kitoweo cha samaki, hata hivyo kampuni ya facebook haikutoa maoni yoyote kuhusu kufungiwa kwa mitandao yake hiyo na pia bado haijajulikana kuwa mtandao huo utafungwa kwa siku ngapi.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use