iPhone 7 Kuja na Memory ya 32GB kwa Size ya Mwisho

iPhone 7 Kuja na Memory ya 32GB kwa Size ya Mwisho iPhone 7 Kuja na Memory ya 32GB kwa Size ya Mwisho

Wataalamu wa mambo ya simu kutoka katika blog mbalimbali za teknolojia nchini marekani wamesikika wakisema huenda simu mpya ya iPhone 7 kuja na internal memory ya GB 32 kwa simu ya mwisho.

Vyanzo hivyo mbalimbali vinaendelea kusema kua kutokana na kuonekana kwa box la nje la simu hiyo likiwa limeandikwa 32gb ni ishara ya kuwa huenda iPhone ikaachana na simu zenye size ya GB16 na kuhamia kwenye GB 32. Hata hivyo kiongozi wa utafiti wa masoko wa kampuni ya IHS Technology Kevin Wang alisikika pia akisema katika kufanya utafiti wake amegundua kuwa simu nyingi sasa zinaelekea kwenye sifa za RAM 2GB pamoja na Memory 32GB hii ikiwa inaonyesha labda ndio njia wanayo-ifuata kampuni ya Apple kwenye simu yao mpya ya iPhone 7 Plus.

Kwa taarifa zaidi endelea kupitia blog ya Tanzania tech ili kupata taarifa ya simu hiyo mpya pia kwa habari motomoto za simu pamoja na teknolojia mbalimbali unaweza kupitia page yetu ya Facebook pamoja na Twitter. Pia kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video pitia page yetu ya Youtube kujifunza kwa vitendo zaidi.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use