Solarin Simu ya Android Inayouzwa Shilingi Milioni 35

Solarin ni Simu ya Bei ghali kuliko zote Duniani ikiwa inauzwa Dollar za Marekani $14,000
Solarin smarphone Solarin smarphone

Je unaujali kiasi gani ulizi wako wa binafsi (Privacy) ? Sirin Labs kampuni ambayo ndio watengenezaji wa smartphone hii ya android ambayo ndio inasemekana kuwa simu ya android ya bei ghali kuliko zote duniani, simu hiyo iliyopewa jina la solarin imetengenezwa maalumu kwa matajiri duniani ambao wanajali ulinzi binafsi.

Inasemekana kuwa ulinzi unaotumiaka kwenye simu hii ni ulinzi unaotumika na jeshi katika ulinzi hii ikiwa na maana baada ya ulinzi wa kitaalamu duniani ambao ni kutoka CIA simu hii ambayo ndio simu ya bei ghali yenye mfumo wa android inategemewa kuingia sokoni leo siku ya tarehe 1 June. Kwa jinsi inavyofanya kazi ni kwamba simu inauwezo wa kuingia katika kipengele maalumu cha ulinzi ama (Safe Mode) ambapo ni lazima uweke alama ya kidole ama fingerprint ili uweze kuingia kwenye sehemu hiyo maalumu baada ya hapo inasemekana kuwa utaweza kutuma meseji na kupiga simu tu na si vinginevyo. Pia simu hiyo inauwezo wa kugundua ni nani ambae amefanya jaribio la kuhack hivyo simu hii ya solarin ina uwezo wa kulinda ulinzi wako binafs na kuangalia ni nani ambae amefanya jaribio la ku-hack simu hiyo.

Advertisement

Sifa za simu hii ni za kawaida sana lakini kinachofanya simu hii kuuzwa kwa bei ya juu sana ni kutokana na uwezo wake wa kutumia moja ya kifaa cha ulinzi wa jeshi kama ulinzi wa simu hiyo, simu hii pia inategemewa kuuzwa kwa watu wenye passport tu na ambao hawana historia yoyote ya ugaidi au kuhusishwa na ugaidi.

Kama umeipenda hii usisite kulike page yetu ya Facebook pamoja na Twitter ili kupata habari mpya pindi zinapotoka,pia kwa kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo unaweza ku subscribe kwenye Youtube Channel yetu hapa.

 

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use