HTC Kuzindua Simu Mpya ya HTC 10 April 12

HTC Kuzindua Simu Mpya ya HTC 10 April 12 HTC Kuzindua Simu Mpya ya HTC 10 April 12

Kampuni ya simu ya HTC ilitoa tangazo hivi karibuni kuwa itaachia toleo lake jipya la smartphone lililotajwa kama HTC 10, wataalamu wa mambo wanasema labda inaweza ikawa ni HTC M10 baada ya toleo liliopita la HTC M9 hata hivyo kampuni hiyo ya simu ilisema itatoa toleo lake hilo jipya siku ya Jumanne April 12 saa 8: 00 AM huko marekani.

Kampuni hiyo iliongeza kwenye tangazo lake kwamba simu hiyo itazinduliwa rasmi kwenye website yao ya htc.com na itakua na vitu mbalimbali kama vile sauti iliyoongezewa ubora kwa wale wanaopenda kusikiliza muziki kwenye simu pamoja na maboresho mengine mbalimbali.

Kama tunavyojua simu za HTC huwa zinakuja na application maalumu ya Beats inayofanya sauti ya muziki kwenye simu yako kuwa nzuri sana na bora, HTC wametangaza kuboresha hilo hata hivyo simu hiyo inatarajiwa kuja ikiwa na kioo cha inch 5.15 kilicho tengenezwa kwa mfumo wa LCD, kamera ya  Mega pixel 12 yenye flash light mbili pamoja na processor ya Snapdragon 820 ikiwa na 3,000 mAh battery.

Advertisement

Kuhusu tukio hili tutawaletea mjumuisho wa habari za simu hii ya HTC 10 pale zitakapo tufikia ikiwa pamoja na tamasha la uzinduzi kama litaonyeshwa live.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use