Share IGTV

Sasa Unaweza Kushare Video za IGTV Kwenye Stories

Mtandao wa Instagram hivi leo umetangaza sehemu mpya kabisa kwenye app yake, sehemu ambayo itakuwa ikikusaidia kuweza kushare video zako za kwenye IGTV kwenda kwenye sehemu ya Stories.

Hapo awali ilikuwa ni rahisi kushare video kwa kuweka link maalum kupitia stories ambayo link hiyo inapo bonyezwa humpeleka mtazamaji kwenye IGTV kwa ajili ya kuangalia video nzima.

Sasa sehemu hiyo mpya itakuwa ni rahisi zaidi kwani, Sehemu hiyo kupitia IGTV itakuwa inapatika kwa kubofya kitufe cha mshale kilichopo pembeni ya kitufe cha comment na kisha chagua sehemu ya “Add video to your story” na baada ya hapo picha ya video ya IGTV itakuwa juu pamoja na link maalum ya kuangalia video kamili pale utakapo bofya picha hiyo.

Kwa sasa sehemu hii tayari ipo kwenye app ya instagram na unaweza kuitumia sasa hivi, kama bado ujaona sehemu hii hakikisha una update app yako ya Instagram na utaona sehemu hii unapokuwa unaangalia video zako ndani ya IGTV.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Lenovo-Z5-Pro sifa na bei
Lenovo Z5 Pro Simu Mpya Kutoka Kampuni ya Lenovo
Next Post
kuzuia kusoma meseji wahtwaspp

WhatsApp Kuja na Njia ya Kuzuia Mtu Kusoma Meseji Zako