Redmi Note 17 Series Imetambulishwa Rasmi 1

Redmi Note 17 Series Imetambulishwa Rasmi

Uzinduzi huu unakuja wakati mfululizo wa REDMI Note umevuka usambazaji wa simu milioni 500 duniani kote

Xiaomi imezindua rasmi REDMI Note 17 series nchini Tanzania, kizazi kipya cha mfululizo wa simu janja zinazouzwa zaidi duniani. Kuna matoleo mawili: REDMI Note 17 4G na REDMI Note 17 Pro Max 5G, toleo la kwanza kabisa la Pro Max katika familia ya REDMI Note.

Redmi Note 17 Series Imetambulishwa Rasmi 2

Uzinduzi huu unakuja wakati mfululizo wa REDMI Note umevuka usambazaji wa simu milioni 500 duniani kote. Simu hizi zimeundwa kudumu kwa miaka mingi, kwa updates za usalama hadi miaka 6 na afya ya betri hadi miaka 6, ili simu yako iendelee kuwa imara na salama kwa muda mrefu.

Redmi Note 17 Series Imetambulishwa Rasmi 3

 OFA ZA UZINDUZI: Nunua leo, upate zawadi BURE!

  • GB 96 BURE kwa mwaka mzima, kwa kila simu ya REDMI Note 17 series
  • Saa janja REDMI 6 Active BURE ukinunua REDMI Note 17 4G
  • Headset Neo BURE ukinunua REDMI Note 17 Pro Max 5G

Betri Inayodumu Siku Nyingi

Redmi Note 17 Series Imetambulishwa Rasmi 4

REDMI Note 17 Pro Max 5G inakuja na betri ya 10,000mAh, betri kubwa zaidi Xiaomi kuwahi kutengeneza, iliyojengwa kwa teknolojia ya REDMI Titan silicon-carbon. Kwa chaji ya 100W HyperCharge, dakika 20 tu za kuchaji zinakupa nguvu ya kutumia simu hadi siku 3.

Uimara wa Hali ya Juu

Pro Max 5G imejengwa kwa REDMI Titan Structure na ina viwango vya IP66, IP68, IP69 na IP69K vya kustahimili maji na vumbi. Imefanyiwa majaribio ya kuanguka kutoka urefu wa mita 3 kwenye sakafu ya mawe, na kukaa ndani ya maji kwa saa 72.

Skrini Kubwa, AI na Kasi

Furahia skrini kubwa ya inchi 6.83, angavu na pana kwa video, gemu na mitandao ya kijamii. Simu hizi zina HyperAI yenye AI Interpret, kutengeneza wallpaper kwa AI na utambuzi wa sauti, pamoja na Circle to Search ya Google. Pro Max 5G inaendeshwa na processor ya Snapdragon 6 Gen 4 kwa kasi na ufanisi kila siku.

Chaguo za Hifadhi

• REDMI Note 17 4G: 8GB + 128GB na 8GB + 256GB

• REDMI Note 17 Pro Max 5G: 8GB + 256GB

Jinsi ya Kupata Ofa yako:

  • Tembelea duka la Xiaomi au muuzaji aliyeidhinishwa aliye karibu nawe
  • Chagua REDMI Note 17 4G au REDMI Note 17 Pro Max 5G
  • Pokea zawadi yako papo hapo na uanze kufurahia GB 96 bure kwa mwaka mzima!

Ofa ni kwa muda maalum tu, wahi sasa kabla hazijaisha!

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Instagram Imetangaza Ujio wa Video Ndefu za Mlalo "Features" 5
Instagram Imetangaza Ujio wa Video Ndefu za Mlalo “Features”