Satelaiti ya Kenya

Video : Jinsi Kenya Ilivyorusha Satelaiti Yake ya Kwanza

Kama wewe ni msomaji wa tovuti ya Tanzania Tech basi lazima utakuwa unajua kuwa wiki hii tarehe 11 mwezi huu wa tano, Kenya ilitangaza kuwa itarusha satelaiti yake ya kwanza. Baada ya tukio hilo kufanikiwa kufanyika hapo siku ya Ijumaa, Jumapili hii ya leo nimekusogezea video ya tukio hilo lilivyokuwa mubashara kutoka nchini Japan. Tukio hilo liliuzuriwa na viongozo mbalimbali wa serikali ya Kenya, pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Jaxa ambao ndio waliorusha satelaiti hiyo.

Baada ya Kenya kufanikiwa kurusha satelaiti yake hiyo ya kwanza nini maoni yako, vipi kuhusu Tanzania..? unahisi inaendana na kasi ya sayansi na teknolojia kama ilivyo nchi ya Kenya tuambie kwenye maoni hapo chini.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
fanya bishara kupitia whatsapp
Jinsi ya Kuuza Bidhaa Kisasa kwa Kutumia App ya WhatsApp
Next Post
App ya Instagram Direct

Sasa Unaweza Kujaribu App ya Kuchati ya Instagram Direct