Ulinzi

Jinsi ya Kuongeza Ulinzi wa Simu Yako na Aina Mpya ya Lock

Karibuni tena kwenye makala hii fupi, kwa kuanza najua wengi wetu tumesha zoea kuwa na ulinzi wa aina flani kwenye simu zetu, lakini kifupi ni kwamba inawezekana kwa sasa unaona ulinzi ulio nao kwenye simu yako hautoshi hivyo unataka kuongeza aina flani ya ulinzi ambayo ni ngumu mtu kuja au kugundua namna ya kufungua simu yako hivyo basi hii ikiwa ndio sababu leo Tanzania Tech tunakuletea aina hii mpya ya lock Screen ambayo na uhakika itakuwa ni ongezeko zuri na bora kwenye ulinzi wa simu yako.

Aina hii mpya ya ulinzi itakupa uwezo wa kulinda simu yako kwa kugusa kioo chako sehemu maalum ambazo wewe pekee ndio utakuwa unajua, hii ikiwa na maana hakuna mtu anaweza kujua ni wapi unagusa ili kufungua simu yako hivyo mtu hatoweza kufanya chochote kile kwenye simu yako, kingine ni kwamba lock hii itakupa uwezo wa kujua anae angalia simu yako kwani simu yako itapiga picha kwa yoyote anaetaka kutoa lock ya simu yako hivyo utakuwa unajua nani alietaka kufungua simu yako,

Vilevile utaweza kufunga simu yako kwa kugusa kioo cha simu yako mara mbili basi hakuna haja ya kubofya kitufe cha kuwasha simu, kifupi ni kwamba lock hii itaongeza ulinzi mara dufu zaidi ya ulinzi ulio uzoea kwa kawaida kwenye simu yako, basi moja kwa moja twende tukangalie njia hii.

Download App hii Hapa kisha endelea kwa kufuata hatua hizi kwenye video hapo chini, kuendelea kujifunza.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Auto Draw
Google Yaleta Auto Draw Programu Mpya Kwaajili ya Kuchora
Next Post
Kompyuta kwenye simu

Jinsi ya Kutumia Kompyuta Yako Kupitia Simu Yako (Smartphone)