Fahamu Haya Kuhusu Game ya Grand Theft Auto VI au GTA 6 1

Fahamu Haya Kuhusu Game ya Grand Theft Auto VI au GTA 6

Tangu siku ya kwanza, game hii imefanya vizuri sana kwenye mauzo na kuvunja rekodi mbalimbali duniani kote

Kama wewe ni mpenzi wa Game basi lazima utakuwa unaijua Game ya Grand Theft Auto au GTA, Game hii ni moja kati ya Game nzuri sana na maarufu duniani ambazo watu wengi wamekuwa wakisubiri kwa hamu kubwa.

Baada ya kusubiri kwa zaidi ya miaka 13 tangu ilipotoka GTA V, hatimaye kampuni ya Rockstar Games imeachia rasmi Game hii mpya ya GTA 6 mnamo Alhamisi ya Novemba 19, 2026 kwa ajili ya PS5 na Xbox Series X|S.

Tangu siku ya kwanza tu ilipotoka, game hii imefanya vizuri sana kwenye mauzo na kuvunja rekodi mbalimbali duniani kote. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie baadhi ya habari kubwa kuhusu GTA 6 hadi sasa tangu game hii ilipoachiwa rasmi.

Kopi Milioni 47 Zimeuzwa Mwishoni mwa Wiki ya Kwanza

Siku ya kwanza tu ilipotoka, GTA 6 ilivunja rekodi kwa kuingiza mauzo ya Dola bilioni 3.79 ndani ya masaa 24 ya mwanzo. Ripoti mpya zinaonyesha kuwa kufikia Jumapili ya wiki ya kwanza, game hii ilikuwa imeshauza takriban kopi milioni 47.8 duniani kote. Kwa sasa ndiyo game inayoongoza kwa mauzo mwaka huu, na karibu asilimia 35 ya PS5 na Xbox Series X|S zote duniani tayari zina game hii ndani.

Wachezaji Milioni 39 Wamecheza Kwenye PlayStation 5

Kampuni ya Sony imetangaza kuwa zaidi ya watu milioni 39 wamecheza GTA 6 kwenye PlayStation 5 ndani ya siku nne za mwanzo tangu itoke. Hii ni rekodi kubwa zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya PlayStation.

Fahamu Haya Kuhusu Game ya Grand Theft Auto VI au GTA 6 2

Wachezaji hao wametumia jumla ya masaa milioni 683 kucheza gemu hii, na karibu asilimia 70 ya PS5 mpya zilizowashwa siku hizo zilianza kwa kucheza GTA 6. Pia maduka mengi makubwa nchini Marekani yameripoti kuwa PS5 zimeisha kabisa stoo kutokana na watu wengi kununua koni hizo ili kucheza game hii.

Wachezaji Waripoti PS5 Kuharibika Kutokana na Matumizi Makubwa ya Umeme

Wakati wengi wakifurahia kucheza GTA 6, baadhi ya wachezaji wanaotumia PS5 wameripoti kuwa PS5 zao zimezima ghafla, kutoa moshi na hata kufa kabisa wakati wakicheza game hii. Mafundi wa kutengeneza PS5 wamefanya majaribio na kugundua kuwa GTA 6 inavuta umeme mwingi sana kufikia wati 274.2 (Watts), wakati game nyingine za kawaida huishia kwenye wati 180 hadi 220.

Fahamu Haya Kuhusu Game ya Grand Theft Auto VI au GTA 6 3

Umeme huu mkubwa pamoja na uzito wa game vinasababisha PS5 za zamani kupata moto sana na kufeli hasa kama feni zake zina vumbi au mfumo wake wa kupoza joto (liquid metal) una tatizo.

Rockstar Watoa Update ya Kwanza Kurekebisha Matatizo ya Game

Siku chache tu baada ya game hii kutoka, kampuni ya Rockstar Games imetoa update ya kwanza (Patch 1.0.2.2) kwa ajili ya kurekebisha matatizo madogo madogo na tatizo la game kujifunga yenyewe (error CE-108255-1) ambalo limekuwa likiwasumbua wachezaji wengi wa PS5. Hata hivyo, baadhi ya wachezaji wamesema kuwa hata baada ya kuweka update hiyo, tatizo la game kujifunga bado linaendelea kujitokeza kwenye baadhi ya PS5.

Na hizo ndio habari kubwa kuhusu GTA 6 hadi sasa tangu game hii ilipoachiwa rasmi, unaweza kutuambia maoni yako kuhusu game hii kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Google Yaja na Search Profile Kwaajili ya Watumiaji wa Mitandao ya Kijamii 4
Google Yaja na Search Profile Kwaajili ya Watumiaji wa Mitandao ya Kijamii