Mamlaka ya maji safi na taka jijini Dar es salaam, leo imetangaza kuja na programu yake mpya ya Android kwaajili ya kusaidia wateja wake wa jijini dar es salaam kwa urahisi zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia ‘TEHAMA’ wa DAWASCO’, Kiula Kingu amesema kuwa lengo kuu la mfumo huu ni kumweka mteja karibu kihuduma.
Hata hivyo akielezea jinsi app hiyo inavyofanya kazi, amesema kuwa mteja wa dawasko au hata ambaye si mteja ataweza kutoa ripoti mbalimbali za kupasuka kwa bomba ili kurahisha wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuzuia matatizo hayo.
App hii kwa sasa inapatika kupitia Play Store na unaweza ku-download app hiyo kwa kubofya link hapo chini, App hii ni bora sana kwani inafanya vitu vingi kwa wakati mmoja na inakupa taarifa zako papo hapo.. ijaribu sasa bofya hapo chini kudownload.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.
Chanzo : Millard Ayo


