Popular Now
Samsung Will Discontinue its Messages app in July 2026 1

Samsung Will Discontinue its Messages app in July 2026

Samsung Yabadilisha Viwango Vya Faragha Ya Simu Duniani Kwa Kuzindua Galaxy S26 Ultra 2

Samsung Yabadilisha Viwango Vya Faragha Ya Simu Duniani Kwa Kuzindua Galaxy S26 Ultra

Sasa Unaweza Kutengeneza Muziki Kupitia Google Gemini 3

Sasa Unaweza Kutengeneza Muziki Kupitia Google Gemini

Kuanzia Leo Tuma Stickers Kwa Kutumia WhatsApp 4

Kuanzia Leo Tuma Stickers Kwa Kutumia WhatsApp

Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu hapa Tanzania hatimaye hivi leo sehemu mpya ya Stikers ndani ya WhatsApp imewezeshwa rasmi, hivyo basi kuanzia leo utaweza kutuma stickers moja kwa moja kupitia App ya WhatsApp.

Mbali na kuwa na uwezo wa kutuma stika pia kupia maujanja mbalimbali sasa utakuwa na uwezo wa kubadilisha baadhi ya picha na kuwa sticker, lakini kabla ya kuangalia hilo labda tungalie kwanza jinsi ya kupata sehemu hii mpya sticker kupitia kwenye app yako ya Android na iOS.

Sasa ili kupata sehemu hii, Sticker unachotakiwa kufanya ni kubofya sehemu ya Emoji kisha kwa chini utaona sehemu mpya ambayo itakuwa na kidoti chekundu kama ndio mara yako ya kwanza kufungua sehemu hiyo, bofya hapo na utona sticker mbalimbali zimefunguka.

Kuanzia Leo Tuma Stickers Kwa Kutumia WhatsApp 5

Chagua sehemu ya emoji kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu kisha chagua sehemu ya mwisho kabisa chini upande wa kulia karibia na GIF, kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.

Kuanzia Leo Tuma Stickers Kwa Kutumia WhatsApp 6

Kuanzia Leo Tuma Stickers Kwa Kutumia WhatsApp 7

Kwa upande wa iOS ni tofauti kidogo na rahisi kuliko Android, kupitia app ya WhatsApp ya iOS fungua app hiyo kisha utaona sehemu ya Sticker pembeni ya chumba cha kuandikia ujumbe, bofya hapo na utapelekwa moja kwa moja kwenye mkusanyiko wa stika mbalimbali.

Kuanzia Leo Tuma Stickers Kwa Kutumia WhatsApp 8

Jinsi ya kutengeneza Sticker zako Mwenyewe

Sasa kama tayari umeshaweza kuona sehemu hiyo mpya basi unaweza kuendelea kuitumia na zaidi ni kuwa unaweza kupakua app mbalimbali za sticker na utaweza kuzitumia moja kwa moja kwenye app ya WhatsApp. Lakini mbali na hayo pia unaweza kutengeneza sticker kutokana na picha zako mwenyewe.

Njia hii ni rahisi sana na unaweza kufanya sasa hivi. Unachotakiwa kufanya ni kudownload App ya Sticker Studio kisha anza kwa kuweka picha yako kisha baada ya hapo kata picha zako kwa kuzungushia duara sehemu unazotaka zibaki, kisha save alafu bofya kutufe cha jumlisha.. Done!! hapo WhatsApp itaweza kufunguka na kukwambia sticker mpya imeongezwa. Unaweza kudownload app hiyo kupitia link hapo chini.

Previous Post
jinsi ya kujua password ya wifi yoyote

Jinsi ya Kujua Password ya WiFi Yoyote (Kwa Kutumia Simu)

Next Post
Jinsi ya kubadilisha muandiko kwenye Samsung au Tecno

Badilisha Muandiko Kwenye Simu za Tecno na Samsung