WhatsApp Stika Stickers

Sasa Unaweza Kutuma Stika kwa Kutumia App ya WhatsApp

Kampuni ya Facebook bado inaendelea kufanya maboresho ya programu zake yaliyo ahidiwa hapo awali kwenye mkutano wa F8 2018, Maboresho mapya kipindi hichi ni maboresho yanayohusu programu ya WhatsApp, maboresho hayo yanahusu sehemu mpya ya stika ambayo sasa watumiaji wataweza kutumiana stika hizo moja kwa moja ndani ya programu hiyo.

Kupitia blog ya yake WhatsApp imeandika kuwa sehemu hiyo itakuja hivi karibuni kupitia mfumo wa iOS na baadae kuja kwenye mfumo wa Android. Kwa mujibu wa blog hiyo sasa utaweza kupata sehemu hiyo kupitia sehemu ile ya emoji inayopatikana kushoto na baada ya kubofya hapo utaona sehemu mpya stika ambayo itakuwa inaonekana pembeni ya GIF.

Kupitia sehemu hiyo mtumiaji ataweza ku-download stika moja kwa moja kabla ya kutumia na pia utaweza kutumia programu mbalimbali za stika ili kuongeza idadi ya stika hizo. Mbali na hayo WhatsApp imetoa nakala maalum ambayo inawahusu wabunifu ambao wanataka kubuni stika kwaajili ya sehemu hiyo mpya ya stika ndani ya WhatsApp.

Kwa sasa kama bado hujapata sehemu hii mpya hakikisha unasasisha (update) toleo jipya la App ya WhatsApp kupitia masoko ya Play Store pamoja na App Store.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Sifa na Bei ya Xiaomi Mi Mix 3
Xiaomi Mi Mix 3 Simu Nyingine Inayokuja na RAM ya GB 10
Next Post
App za kusikiliza muziki kwenye android

App Nzuri za Kusikiliza Muziki (Music Player) Kwenye Android