Linapokuja swala la kuanzisha twebsite au tovuti iliyo bora ni wazi kuwa gharama ni kubwa sana tena hasa kama unataka kuwa na tovuti yenye muonekano mzuri na yenye kufanya kazi vizuri. Lakini ni wazi kuwa kwa hapa Tanzania sio kila mtu mwenye uwezo wa kuanzisha website kwa kutumia pesa nyingi, hivyo ni wazi kuwa kunaitajia njia ya ziada kuweza kusaidia kila mmoja kuanzisha website bila kutumia gharama yoyote.
Kuwezesha hayo leo Tanzania Tech tunakuletea njia nzuri sana ya kuweza kukusaidi kutengeneza website bure kabisa bila kutumia gharama yoyote. Vilevile njia hii itakusaidia kuanzisha website au tovuti, yaani utakuwa na uwezo wa kuwa na domain yako yenye jina unalolitaka na hutolipia domain hiyo wala hutolipia gharama zingine zozote, kikubwa ni wewe kuwa na Internet na kufuatilia makala hii hadi mwisho.
Kumbuka njia hii unaweza kutumia kutengeneza website kwaajili ya biashara au kama ni website au tovuti ya habari kama Tanzania Tech, unaweza kufanya hivyo pia. Kitu cha muhimu ni kuhakikisha unachagua template nzuri ambayo itafanya website yako iweze kuonekana vizuri. Unaweza kusoma makala hii hapa ili kujua jinsi ya kuweka templent pamoja na kupata Template hizo za bure.
Baada ya njia hii nitaenda kuonyesha njia ya kutengeneza App kwaajili ya hiyo tovuti yako, njia hiyo itaitaji kuwa na programu ya Android Studio hivyo basi kama ungependa kujifunza maujanja hayo unaweza kupakua programu hiyo kwaajili ya somo au maujanja yanayofuata. Hakikisha una subscribe kwenye channel ya Tanzania Tech ili kuhakikisha hupitwi na maujanja hayo.


