tengeneza tovuti kwa simu

Tengeneza Tovuti Kupita Simu Yako kwa Kutumia App Hii

Ukweli ni kuwa iwe ni mfanya biashara au hata mfanyakazi wa kampuni fulani tovuti ni kitu cha muhimu sana, tovuti ni kama utambulisho maalum wenye mkusanyiko wa taarifa zako za muhimu ambazo unataka kushiriki na jamii iliyo kuzunguka. Lakini kunatatizo, sio kila mtu anaweza kutengeneza tovuti, wengine hawana hata kompyuta za kuweza kuwasaidia kufanya hivyo. Lakini sasa suluhisho limepatikana.

Kampuni moja inayo chipukia ya nchini marekani inayoitwa Universe, imeanzisha njia mpya na rahisi ya kutengeneza tovuti kupitia simu yako ya mkononi. Njia hiyo ambayo inatumia programu au App maalum inakupa uwezo wa kutengeneza tovuti za aina mbalimbali kwaajili ya biashara, tovuti binafsi na tovuti nyingine kama hizo.

Kupitia App hiyo utaweza kutengeneza kurasa za tovuti yako pia utaweza kuweka link zako za mitandao ya kijamii pamoja na kuandika maelezo mafupi kuhusu wewe au biashara yako. Vilevile kupitia programu hii utaweza kutengeneza tovuti yenye domain au kioleo cha bure cha onuniverse.com yaani tovuti yako itakuwa na link kwa mfano tanzaniatech.onuniverse.com

Mbali na hayo utaweza kuchagua domain ya kulipia na kuiweka sambamba na tovuti yako uliyo tengeneza kwa kutumia App hiyo, App hiyo ambayo kwa sasa inapatikana kwa watumiaji wa iOS inakupa vifaa mbalimbali vya wewe kuweza kutengeneza tovuti yako ndani ya dakika moja tu. Unaweza kuangalia tovuti niliyo tengeneza kwa simu kwa kubofya HAPA. Unaweza kupakua programu hiyo kwenye simu yako ya iPhone na kuanza kutengeneza tovuti yako kwa urahisi zaidi.

Kwa watumiaji wa simu za Android bado hakuna taarifa lini programu hiyo itakuja kwenye mfumo huo lakini tuendelee kusubiri pengine programu hii itakuja siku za karibuni na bila shaka tutakujuza kupitia hapa hapa Tanzania Tech.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Dark Theme Youtube
YouTube Android na iOS Kuja na Sehemu Mpya ya Dark Theme
Next Post
 Stephen Hawking

Mtaalamu wa Teknolojia Stephen Hawking Afariki Dunia Leo