Facebook Matangazo

Facebook Kuonyesha Matangazo Yake kwa Kila Mtu

Mtandao maarufu wa kijamii wa Facebook hapo jana ulitangaza kupitia blog yake kuwa sasa unaanza kuonyesha matangazo yake kwa watu wote hata wale ambao sio watumiaji wa mtandao huo, facebook ilichukua hatua hiyo baada ya kuona fursa kwenye sehemu hiyo ya matangazo ambapo mwaka jana ilizalishia kampuni hiyo zaidi ya bilioni 5 za kimarekani.

Kipindi cha nyuma matangazo hayo yalikua yakionekana kwa watumiaji wa facebook pekee lakini sasa tumeamua kupanua  huduma hii ili kusaidia watumiaji wetu kupanuka zaidi na kwa urahisi kabisa, pia tutatoa nafasi kwa waandishi na watangazaji kufika mbali kwa kuwa saidi kwa upande wa kutafuta masoko ili kutengeneza jamii iliyo bora zaidi, alisema Andrew Bosworth makamu wa rahisi wa matangazo na biashara hapo facebook.

Kwa taarifa zaidi soma blog ya facebook hapa Facebook Business Blog

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
TV 40 and 42 Inch
Hizi Hapa TV Bora za Inch 40 na 42 Kwa Mwaka (2018)
Next Post
twitter

Twitter Yaondoa Picha Kwenye Hesabu ya Maneno