in

Mambo Hatari Ambayo Hutakiwi Kufanya Mtandaoni

Kua mbali na mambo haya kama unataka kuwa salama mtandaoni

Mambo Hatari Ambayo Hutakiwi Kufanya Mtandaoni

Ni kweli kwamba internet mtandao ni ulimwengu mpya na ambao una kila kitu endapo unajua mahali pakuangalia. Kutokana na Internet kuwa na kila kitu ni vyema kujua mambo kadhaa ya msingi ambayo kwa maoni yangu hauruhusiwi kufanya na endapo ukifanya basi usisema sijakwambia.

Usitumie (Password) Nywila ya Aina Moja

Mambo Hatari Ambayo Hutakiwi Kufanya Mtandaoni
Password au Nywila ni sehemu ya Internet kwani karibia nusu ya huduma zinazotolewa mtandaoni zina tolewa baada ya kujisajili. Sasa wakati una jisajili kuwa muangalifu sana usitumie password moja kwenye kila tovuti au app unayo tumia mtandaoni.

Mara nyingi hasa hapa kwetu Tanzania watu wame kuwa wavivu kuweka password za aina tofauti kwa kuhofia kusahau, wengine wanaweka password ambazo ni namba za simu au mwaka wa kuzaliwa, hii ni hatari sana na ni vyema kuacha tabia hii haraka.

Usitumie WiFi ya Pamoja Isiyokuwa na Password

Mambo Hatari Ambayo Hutakiwi Kufanya Mtandaoni

Ni kweli kwamba hakuna kitu chochote cha bure kisicho kuwa na gharama, Wengi wetu hupendelea kutunza fedha kwa kutumia huduma za bure lakini ni wazi kuwa mara nyingi tunapata hasara kuliko faida.

WiFi ya bure ni baadhi ya huduma inayoweza ikiwa inatolewa na mtu au watu kwa ajili ya kuongeza biashara, lakini pia ni vyema kuwa muangalifu na WiFi hizi kwani nyingine hutumika vibaya kuchukua data za muhimu kutoka kwenye simu au kifaa chako au wakati mwingine hutumiwa kuweka virus ambavyo vinaweza kufanya mambo ambayo usingependa yakukute.

Usiamini Watu Usio Wajua Mtandaoni

Mambo Hatari Ambayo Hutakiwi Kufanya Mtandaoni

Hapa kwetu Tanzania nadhani kila mtu analo somo la usiamini usie mjua kichwani, lakini kutokana na utandawazi ni ngumu sana kumjua mwema au muovu kwa sababu wote wanasura moja. Kutokana na hilo ni vyema sana kuwa muangalifu hasa huku mtandaoni na usimuamini yoyote usiyemjua, tena hasa pale inapokuja kwenye maisha yako binafsi.

Njia Bora ya Kuondoa Background kwenye Picha (Android)

Kumbuka mtu yoyote anaweza kuwa mtu hatari na wakati mwingine watu wabaya hutumia akili nyingi sana kuweza kupata wanacho kitaka hivyo umakini ni jambo la msingi sana pale unapokuwa mtandaoni.

Usiandike au Kuweka Kila kitu Binafsi Mtandaoni

Mambo Hatari Ambayo Hutakiwi Kufanya Mtandaoni

Kuwa na akaunti za mitandao yote ya kijamii sio kitu kibaya, lakini pia ni vyema kuwa makini na usiweke kila kitu cha maisha yako kwenye internet. Kuna watu hapa Tanzania unaweza kujua anakaa mtaa gani, sehemu gani na hata sasa hivi yuko wapi, hii ni hatari sana. Ukiwa kama mtu unaejielewa huna haja ya kuweka maisha yako yote kwenye mitandao mbalimbali kwani hii inatoa mwanya kwa watu mbalimbali kuweza kukufuatilia kwa namna moja ama nyingine.

Kuwa Makini Unacho Pakua (Download)

Mambo Hatari Ambayo Hutakiwi Kufanya Mtandaoni

Kutumia Internet au Mtandao bila ku-download kitu ni sawa na gari lisilo na dereva, kwa mujibu wa tovuti ya kaspersky ni vyema kuwa makini sana na tovuti ambazo unadownload vitu kwani unaweza kupakua vitu visivyo salama au vyenye virusi ambavyo vinaweza kuharibu kifaa chako au kuchukua data zako za muhimu. Kitu cha muhimu kama unaona tovuti huiamini basi unaweza kutumia anti-virus au huduma kama virustotal.com ku-scan file zozote kabla ya kuweka kwenye kifaa chako.

Usitembele Tovuti au App Zenye Kuvunja Sheria

Mambo Hatari Ambayo Hutakiwi Kufanya Mtandaoni

Unaweza kudhani vitu hivi vipo kwenye Movie pekee lakini ni kwambie kama una mchezo wa kutembelea tovuti zenye kuvunja sheria kwa namna moja ama nyingine ipo siku yata kukuta. Mara nyingi tovuti hizi huwa zinaruhusu mambo ambayo ni kinyume na sheria hivyo labda kama wewe ni mtaalamu wa mambo haya na unatumia programu bora ya VPN basi unaweza kuendelea kujificha hasi siku ya 40 maana za mwizi ni 41.

Jinsi ya Kufuta kwa Haraka Majina Yaliyo Jirudia

Usitumie Mtandao (Internet) Muda Wote

Mambo Hatari Ambayo Hutakiwi Kufanya Mtandaoni

Ni kweli kwamba Internet ina vitu vingi sana na ambavyo unaweza kutumia kuongeze uelewa wako ikiwa pamoja na kupata elimu kwa urahisi, Lakini internet kama ilivyo vitu vingine inaweza kuwa na urahibu wa hali ya juu kiasi kwamba kila muda unakuwa mtandaoni na kushindwa kufanya mambo mengine ya msingi kwenye maisha yako. Wakati mwingine unaweza kupata matatizo kama vile ugonjwa wa kupenda smartphone ambao huu mara nyingi husababishwa na uwepo wa Internet.

Usitumie Google Kutafuta Vitu Vinavyo Kiuka Sheria

Mambo Hatari Ambayo Hutakiwi Kufanya Mtandaoni

Ukweli ni kwamba hakuna usalama wa asilimia 100 mtandaoni, kila unachofanya kwa namna moja ama nyingine kina hifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya baadae, unaweza kuona huduma kama za Google zinakutaarifu kuwa hakuna data zako zinazo hifadhiwa lakini kwenye ulimwengu huu wa sasa wa matangazo ya kidigitali ni muhimu kujua Data is Power.

Kama kungekuwa na usiri wa aslimia 100 kampuni kama Facebook, Google na kampuni nyingine zenye huduma za matangazo zisingekuwa zinafanya kazi hadi sasa. By the way… asilimia kubwa za mapato ya Facebook na Google zina tokana na Matangazo…

Jua Internet ni Nzuri na Ni Mbaya Sana

Mambo Hatari Ambayo Hutakiwi Kufanya Mtandaoni

Mwisho kabisa haya ni maoni yangu kwako msomaji wangu, kama unadhani internet ni sehemu nzuri basi ni jambo jema sana.. lakini pia naomba uweke mawazo haya kichwani kwako na hakikisha unajua kuwa Internet pia ni mbaya sana kiasi kwamba ukiitumia vibaya unaweza kuaribu maisha yako kwa namna nyingi sana. Hakikisha mawazo haya yanakuwa kichwani kwako kila mara unapotaka kufanya jambo mtandaoni.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment