in

Tecno Yazindua CAMON 19, Yenye Kupiga Picha Kali Hasa Usiku

Hizi Hapa Simu Mpya za TECNO Camon 19

Tecno Yazindua CAMON 19, Yenye Kupiga Picha Kali Hasa Usiku

Dar es Salaam, Tanzania, 06 Julai, 2022– TECNO Mobile Tanzania, chapa ya simu za kisasa na bora duniani ambayo imekuwa ikitoa teknolojia ya kisasa zaidi kwa watumiaji, leo imetangaza uzinduzi wa toleo lake la CAMON 19 kwa kushirikiana na Vodacom.

Toleo la CAMON 19 limekuja ili kukabiliana na changamoto za kitamaduni zinazohusishwa na upigaji picha wakati wa usiku na hali ya mwanga hafifu, ikiwa na vipengele kama vile teknolojia ya upigaji picha za usiku ya 64MP na bezel ndogo zaidi ya 0.98mm ya tasnia.

TECNO na Vodacom wanaungana kuhakikisha wanawapatia wateja wao simu ya kisasa yenye kifurushi cha intaneti cha 96GB BURE kwa muda wa mwaka mzima ili sio tu kuinua ujuzi wao wa kupiga picha, bali pia kuwasaidia kuhamia katika ulimwengu wa kidijitali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Uhusiano wa TECNO Bi. Prisca Ernest alisema, “Tunajivunia kutambulisha toleo jipya la CAMON 19 na kuendelea kuimarisha dhamira yetu ya kukua na kuwekeza zaidi katika nyanja za teknolojia na ubunifu.”

Tecno Yazindua CAMON 19, Yenye Kupiga Picha Kali Hasa Usiku

Afisa uhusiano wa TECNO akizungumza kuhusu sifa kuu za CAMON 19

Bi Prisca alisisitiza zaidi juu ya teknolojia ya upigaji picha za usiku, alisema, “Simu yetu ya CAMON 19 inakuja na kamera kuu ya 64MP na sensor ya RGBW / glasi. Kamera hii ya CAMON 19 imeleta viwango vipya vya kupiga picha angavu na halisi hata nyakati za usiku.

Muundo Wa Infinix Zero Ultra 3D Curved Washangaza Wengi

Aliongeza pia,” TECNO CAMON 19 ina bezel nyembamba sana ya 0.98mm, ikiwa na skrini ya inchi 6.8 FHD+ inayotoa uzoefu usio na kifani.”.

Zaidi ya hayo, alisema kuwa TECNO CAMON 19 Pro inaendeshwa na chipset ya MediaTek Helio G96 yenye skrini bora, nguvu zaidi ya kuchakata picha na kasi ya juu zaidi.

Pia alitaja vipengele vingine vya kuvutia vya CAMON 19 ikiwa ni pamoja na muundo maridadi, nafasi kubwa ya 256+8GB na 120Hz.

Tecno Yazindua CAMON 19, Yenye Kupiga Picha Kali Hasa Usiku

Sifa kuu za simu ya TECNO CAMON 19

                

Muonekano wa simu ya TECNO CAMON 19 katika rangi mbalimbali

Afisa Mkuu wa Biashara wa TECNO, Bi. Salma Shafii, alisema, “Lengo la kushirikiana na Vodacom ni kukuza maisha ya kidijitali katika jamii ya Watanzania, kuongeza idadi ya simu za kisasa na watumiaji wa intaneti sokoni kupitia uzinduzi wa vifaa vya simu kama vile toleo jipya la CAMON 19”.

Bi Salma aliongeza kuwa, “Nina furaha kutangaza kwamba kila mteja atakayenunua TECNO CAMON 19 atapata intaneti ya mwaka 1 bure ya GB 96 kutoka Vodacom na zawadi nyingine za papo kwa hapo ikiwemo spika ya Bluetooth, power bank na tiketi ya sinema kutoka Century Cinemax.”

Shina Zawadi Kibao Kupitia TECNO Spark 9 na CAMON 19

Tecno Yazindua CAMON 19, Yenye Kupiga Picha Kali Hasa Usiku

Afisa mkuu wa Biashara wa TECNO akizungumza kuhusu faida za kununua simu ya TECNO CAMON 19

Vile vile, meneja wa masoko wa TECNO Bw. William Motta, alisema, “Toleo la CAMON 19 limekuja katika aina tatu za ambazo ni CAMON 19, CAMON 19 Pro na CAMON 19 Pro 5G. Bei zitakuwa 450,000 kwa CAMON 19 (128+4GB), 510,000 kwa CAMON 19 (128+6GB), 660,000 kwa CAMON 19 Pro, na 790,000 kwa CAMON 19 Pro 5G.

Tembelea duka lolote la TECNO au duka la Vodacom ili kupata uzoefu wa simu hii mpya. Pia unaweza kuagiza mtandaoni kupitia INALIPA:

Tecno Yazindua CAMON 19, Yenye Kupiga Picha Kali Hasa Usiku

Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0744 545 254 au 0678 035 208.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.